Juma Kaseja Aula Serengeti Boys.Golikipa wa  zamani wa timu ya Taifa Star na Vilabu vya Simba,Yanga,Mtibwa Sugar na Mbeya City Juma kaseja ameteuliwa kukaimu kwa muda nafasi ya kocha msaidizi wa Serengeti boys Sebastian Mkoma katika kambi itakayowekwa nchini Madagascar pamoja na mchezo dhidi ya Afrika kusini.

Taarifa ya kuteuliwa kwa Kaseja kukaimu nafasi hiyo imethibitishwa na Msemaji wa TFF Alfred Lucas katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 25.

“Kuna kozi mbali mbali ambazo zinaendelea sasa hapa nchini. Kocha msaidizi wa Serengeti Boys Sebastian Mkomwa pamoja na Mohamed Mwarami hawatakuwepo katika msafara huo hivyo Juma Kaseja atakuwa msaidizi wa Kocha bakari Shime” amesema Alfred.

Mbali na kuwa msaidizi wa Shime, Kaseja atakuwa pia ni kocha wa makipa.

Wachezaji wa Serengeti Boys

Kikosi cha Serengeti Boys kinataraji kuondoka nchini alfajiri ya kesho Julai 26 kuelekea nchini Madagascar kwa ajili ya kuendelea na kambi ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana dhidi ya Afrika kusini utakaochezwa mapema mwezi ujao.

Safari Sertengeti Boys kwenda Madagascar ni ahadi iliyotolewa na rais wa TFF Jamal Malinzi wakati timu hiyo ilipokua katika mchakato wa kucheza mchezo wa awali wa kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Shelisheli, ambapo iliahidiwa kwenda kuweka kambi nchini Madagascar kama wangeshinda mchezo huo, jambo ambalo lilitimia.

SERENGETI BOYS KIKOSI

Jumla ya wachezaji 19 ndio watakaoelekea Madagascar wakiongozwa na Meneja wa timu Ayubu Nyenzi, Kocha mkuu Bakari Shime, daktari wa timu Sheikh Ngazija, pamoja na mtunza vifaa Andrew Andrew.

Post a Comment
Powered by Blogger.