JESHI LA POLISI LIMEKAMATA MADEREVA WA PIKIPIKI.
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda 305 kwa kukiuka sheria za barabarani kwa kutovaa kofia ngumu, kutokuwa na leseni na kupakia abiria zaidi ya mmoja maarufu kama mishikaki.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Wilbrod Mutafungwa amesema kuwa madereva hao wanashikiliwa kufuatia msako uliofanyika kuanzia Julai 1-10, mwaka huu ambapo 35 kati yao wameshafikishwa mahakamani.