Huyu Hapa Anayelipwa Kwa Kubikiri Watoto Ili Kuondoa Mikosi.

Ukishangaa ya Musa utayaona ya filauni-huku nchini Malawi mzee mmoja analipwa kwa kubikiri Watoto, wanaume hao wanajulikana kwa jina la Fisi. katika utamaduni ulidhoeleka katika jamii moja nchini humo haithamini ubirika wa watoto kama jamii zingine Afrika.
fisi kumbikiri binti punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza [kuvunja ungo] huku wakiamni kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi katika jamii yao.
cha kushangaza zaidi kuwa Fisi ama wanaume wanaobikiri mabinti kuwa huchaguliwa na wazazi wao wenyewe kuwaondolea mikosi
Na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya kutambulishwa kwa fisi.
Amini usiamini hao mafisi hulipwa takriban dola $7 kwa kila kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14.
Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva anasema kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi, kwa sababu ni wengi.
''Kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104," amesema. ''Hii ndiyo tamaduni yetu''.
''Hapa mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa mumewe''.
''Mwanamke akiavya mimba pia kabla hajarejelea maisha yake ya kawaida ama hata kushiriki ngono na mwanamume mwengine lazima aje kwangu nimsafishe," alisema fisi huyo.
Aniva ambaye ana umri wa takriban miaka 40 ana wanawake wawili na watoto 5.
Anasema kuwa pale anaposhiriki ngono na watoto hao huwa anapewa muda wa siku 3 hivi kumsafisha na kumuondolea mkosi.
Kulingana na tamaduni zao, ikiwa mwanamke ama binti anakataa asibikiriwe huwa wanaamini kuwa jamaa zao watafuatwa na mikosi na magonjwa.
Post a Comment
Powered by Blogger.