HUU NDO MVUTANO WA TRA NA BoT KUHUSU VAT.


Wakati Mamlaka ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiitaka Benki Kuu Tanzania (BoT) kuzichukulia hatua taasisi za kifedha zilizopandisha gharama za huduma kwa madai ya ongezeko la kodi ya thamani ya asilimia 18, Benki Kuu imesema kuwa taasisi hizo za fedha hazijakosea kufanya hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata alisema kuwa benki hizo zinakosea kupandisha gharama kwa wateja wake na kua TRA na Wizara ya Fedha na Mipango ambao ndiyo wasimamizi wa sheria hiyo hawajatoa mwongozo kwa benki hizo kupandisha gharama.

Aliendelea kutanabaisha kuwa, ongezeko la VAT 18% litatozwa kwenye fedha aliyokuwa akikatwa mteja mwanzoni wakati anapotumia huduma ya kifedha kwa sababu benki hizo awali zilikuwa zikimkata mteja bila kulipa kodi ya faida wanayopata.

Wakati huo huo, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu amesema yeye haoni kosa kwa benki hizo kufanya hivyo kwani zina wajibu wa kuwajulisha wateja wake kuhusu ongezeko hilo la ngarama, na hayo ni matakwa ya sheria.

Mvutano huu umetokana na marekebisho ya Sheria ya Fedha yaliyopitishwa na Bunge ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango alisema kuwa taasisi za fedha zitakatwa asilimia 18 ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika ada zinazowatoza wateja wake pindi wanapotumia huduma hiyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.