Hizi Hapa Tetezi Za Usajili Barani Ulaya.

TETESI KUTOKA BARANI ULAYA:
Wakala wa Paul Pogba bado hajasema ni lini tarehe ya mwisho mchezaji huyo anatakiwa awe tayari amekwisha kamilisha uhamisho wa kwenda Manchester United, lakini pande zote mbili zinataka kukamilisha dili hilo haraka iwezekanavyo. (Chanzo Manchester Evening News)
Pogba huenda akaamua kubaki Juventus kwa sababu atapata nafasi ya kushiriki UEFA Champions League na mabingwa hao wa Serie A, ile hali Manchester United watashiriki daraja la pili Europa League. (Chanzo Times)
Manchester United wanafikiria kufanya uhamisho wa kiungo wa Liverpool Joe Allen, 26, lakini mchezaji huyo wa Wales ananyatiwa pia na Swansea City. (Chanzo South Wales Evening Post)
Wakati huo huo, Liverpool wanamfukuzia kiungo wa Newcastle Georginio Wijnaldum, 25. (Chanzo Telegraph)
Meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte amesema winga Juan Cuadrado, 28, yuko kwenye mipango yake ya sasa, baada ya kuitumikia Juventus kwa mkopo msimu uliopita. (Chanzo Daily Star)
Klabu ya Roma ya nchini Italia imesema kuwa beki wake Kostas Manolas, 24, hauzwi. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugiriki alikuwa akihusishwa na kuhamia aidha Arsenal au Chelsea. (Chanzo Evening Standard)
Manchester City wamepewa ofa ya kumsajili beki wa Juventus Leonard Bonucci, 29 – lakini mabingwa hao wa Juventus wanataka wapewe paundi millioni 50. (Chanzo Manchester Evening News)
City wanataka pia kushinda na mahasimu wao Manchester United kwenye kuipata saini ya beki wa West Ham Reece Oxford, 17. (Chanzo Sun)
Barcelona na Real Madrid wote wameonyesha nia ya kumtaka kiungo wa Ureno Andre Gomes, ambaye ametajwa kuwa na thamani ya paundi millioni 54 na klabu yake ya Valencia. (Chanzo Super Deporte)
Riyad Mahrez, 25, anataka kukamilisha “ndoto” ya kuhamia kwa mabingwa wa Hispania Barcelona baada ya kukataa mkataba mpya na Leicester City. (Chanzo Sun)
Lakini Claudio Ranieri anauhakika kuwa Mahrez hataondoka King Power Stadium. (Chanzo Daily Star)
Post a Comment
Powered by Blogger.