Hillary Clinton Asema Donald Trump Hawezi Kutatua Matatizo Ya Wamarekani.
![]() |
Mgombea Urais wa Marekani Hillary Clinton. |
Alitoa wito kwa wanachama wote wa Democratic
kuungana naye huku akimkebehi mpinzani wake wa chama cha Republican,
Donald Trump, katika madai yake kuwa ni yeye pekee anayeweza
kuyasuluhisha matatizo ya Marekani.
Alisema kuwa Wamarekani hufanya kazi kwa pamoja kyatatua yote yanayonufaisha taifa.
Awali, bintiye Chelsea Clinton alikuwa ametoa hotuba na kumsifu sana mamake. Alisema ni mwanamke ambaye huwa hasahau anawapigania akina nani.
"Watu huniuliza kila wakati, huwa anawezaje kufanya haya? ... ni kwa sababu huwa hawasahau watu anaowatetea," amesema.
"Najua kwa moyo wangu wote kwamba mamangu atatufanya tujionee fahari."