HII HAPA REKODI YA ITALIA NA UJERUMANI LEO ROBO FAINALI EURO 2016 UNAJUA NANI YUPO JUU YA MWENZAKE.


Na Mahmoud Rajab.

Robo fainali ya tatu inapigwa inapigwa leo ambapo miamba miwili ya Ulaya Ujerumani na Italy watakuwa na kibarua kigumu kutafuta nafasi ya kutinga nusu fainali, mchezo utakaofanyika kunako dimba la Matmut Atlantique lililopo jijini Bordeaux majira ya saa nne za usiku.

Taarifa muhimu za kila timu.

Ujerumani wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na kikosi kamili baada ya wachezaji wao Jerome Boateng, Julian Draxler na Sami Khedira kuwa kupona majeraha yao madogo yaliyokuwa yakiwasumbua.
Italy watakuwa na hati hati ya kutomtumia kiungo wake Daniele De Rossi, ambaye anasumbuliwa na jeraha la paja alililopata katika mchezo dhidi ya Uhispania.
Mbadala wake sahihi Thiago Motta naye hatakuwepo kutokana na kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja kufuatia kupata ladi mbili za njano, huku winga Antonio Candreva pia akikosekana.
Endapo De Rossi atashindwa kabisa kucheza mchezo wa leo, basi nafasi yake itabidi izibwe na Stefano Sturaro.

Jambo la hatari zaidi ni kwamba wachezaji takriban 11 wa Italy wana kadi za njano. Wachezaji hao ni Andrea Barzagli, Leonardo Bonucci, Gianluigi Buffon, Giorgio Chiellini, Daniele De Rossi, Mattia De Sciglio, Eder, Lorenzo Insigne, Graziano Pelle, Salvatore Sirigu na Simone Zaza. Na endapo watapa kadi nyingine leo tafsiri yake ni kwamba wataukosa mchezo wa nusu fainali endapo timu yao itafuzu.
Kwa upande wa Ujeruamni Boateng, Khedira, Mats Hummels, Joshua Kimmich na Mesut Ozil wote wana kadi za njano.

Preview.
Italy wamekutana na Ujerumani mara nane katika michuano mbalimbali mikubwa duniani na hawajawahi kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika michezo minne ya mtoano waliyokutana , wamewafunga Ujerumani kwenye mecho zote nne, huku ya mwisho ikiwa ni ile ya nusu fainali ya Euro mwaka 2012 ambapo Italy walishinda mabao 2-1.
Ni rekodi nzuri sana kwa Italy lakini inayochoma kwa Ujerumani. Lakini safari hii Ujerumani wanaonekana kuja na ‘mentality’ tofauti kabisa kuelekea mchezo wa leo.

“Hatuna hofu na Italy, kwa sababu ni timu tofauti kwa sasa na nadhani kwa sasa hatufikirii chochote juu ya masuala yaliyopita,” kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema.

“Tunahitaji kahawa ya baridi na tutahakikisha inakuwa na ladha nzuri sana siku ya Jumamosi (leo),” ameongeza.
Katika mchezo wao wa kirafi uliochezwa mwezi March Ujerumani walionesha ukomavu wa aina yake baada ya kuwatungua Italy mabao 4-1.

Moja ya vita makubwa leo jijini Bordeaux itakuwa katika safu ya ulinzi. Italy wameruhusu goli moja tu mpaka sasa tena goli ambalo lilifungwa wakati mabeki wao visiki maarufu kama BBC Andrea Barzagli, Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini hawakucheza pamoja (kwenye mchezo dhidi ya Republic of Ireland).

Safu ya ulinzi ya Ujerumani nayo si ya kugusa kwani timu timu pekee mpaka sasa kwenye michuano hii ambayo nyavu zake haziguswa na timu yoyote.

Takwimu muhimu katika mechi walizokutana.
Ujerumani.
Italy.
Post a Comment
Powered by Blogger.