HEKIMA NI NGUVU ZAKE MWENYE HEKIMA,ZAIDI YA WAKUU KUMI WALIOMO MJINI.

HEKIMA NI NGUVU ZAKE MWENYE HEKIMA, ZAIDI YA WAKUU KUMI WALIOMO MJINI
Imani Kelvin Mbaga's photo.
Ukiona katika uongozi wako kila wakati unapishana na unaowaongoza na kubishana nao huku ukitumia nguvu kubwa kuhalalisha uhalali wako wa kuwa kiongozi basi ujue kuna walakini ktk uongozi wako.
Hivi majuzi Uingereza wamepiga kura kujiondoa ktk umoja wa ulaya na waziri mkuu David Cameron ametangaza kuachia ngazi siyo kwa sababu hana uwezo wa kuongoza lkn anahisi amepoteza ushawishi ndiyo maana wapiga kura hawakufuata mawazo yake.
Yapo mambo mengi yanayotokea hapa kwetu ambayo endapo tungekuwa tunatanguliza HEKIMA badala ya nguvu tungefika mbali sana.
Nilipoisikiliza hotuba ya mh rais wa TFF, mzee wangu Jamal Malinzi nikagundua namna shirikisho letu linavyoendeshwa kwa kubahatisha na hiyo ikanikatisha tamaa kbs.
Nakubaliana naye katika yote aliyoyasema lkn nikapata shaka juu ya uhalisia wa yote hayo.
Kwamba TFF ndiye msimamizi mwenye mamlaka hapa nchini kwa mujibu wa katiba za FIFA na CAF hili liko wazi hali hitaji kbs digrii ili kuling'amua.
Lakini kuja kutuomba radhi baada ya uzembe, ubabe, kukomoana na kuvimbiana ambako kunaweza kutugharimu hiihaikubaliki.


Nani asiyejua kuwa michezo ni biashara na kama ni biashara basi majadiliano hutumika zaidi ili kufikia muafaka?
Kinachoshindikana hasa kukaa chini, kujadili na hatimaye kuja na muafaka unaomnufaisha kila mmoja ni nn?.


Mabishano kati ya TFF na vilabu hayajaanza leo, au kwa Yanga tu.
Mwanzoni mwa msimu walitaka kukata 5% ya mapato ya milangoni kwa madai ya kukuza soka la vijana, sakata lililo mpeleka jela ya soka wakili Ndumbaro.
Ni TFF hao hao wanaotuhumiwa kupanga matokeo ya ligi daraja la kwanza hadi kuivuruga kbs
.Ni TFF hao hao wanaotuhumiwa kuvuruga ratiba ya ligi na kusababisha malalamiko mengi.
Hatusemi juu ya kuvuruga chaguzi za wanachama wao kwa maslahi yao binafsi.
Haya ni baadhi ya malalamiko yanayoinyima TFF uhalali wa kuaminiwa hata wanapokuja na hoja ya msingi.
Mimi kama baba mwenye hekima siwezi kwenda kubishana na mtoto wangu mtaani wala kufanya jambo lolote la kumkomoa pale ninapotofautiana nae.
Kwa shirikisho kubwa la soka kama TFF kuanza kubishana na Murro kwenye vyombo vya habari ni kujivunjia heshima na kujishushia hadhi.
Moja kati ya udhaifu mkubwa wa TFF hivi sasa ni juu ya kuendesha michakato mbalimbali kuanzia ajira za ndani, jinsi ya kupata wadhamini, haki za runinga nk.
Msipokuwa wazi kwa mali na haki za watu hiyo ni dhambi itakayowatafuna miaka nenda na miaka rudi na historia kuwahukumu.
Kama mngekuwa na utaratibu wa kutumia meza ya mjadala ktk kuendesha mambo yenu haya yote yasingefika huku yalikofika.
Tujifunze kwa makosa na tuwe tayari kubadilika panapobidi. Tuiweke mbele hekima kwakuwa, hekima ndiyo nguvu ya mwenye hekima.


‪#‎Imani‬ Kelvin Mbaga
Post a Comment
Powered by Blogger.