Haya Hapa Maoni Ya Wasomi,Wanaharakati Na Wanasiasa Juu Ya Uteuzi Wa Rais Magufuli.Baada ya Rais kuendelea kuunda serikali ya awamu ya tano baada ya kuteua wakurugenzi wa Halmshauri mbalimbali, wasomi, wanasiasa wanaharakati wametoa maoni mbalimbali kuhusu teuzi hizo.
Baadhi wameeleza kuwa sio sahihi kwa Rais Magufuli kuteua makada wa CCM kuwa wakurugenzi wa wilaya kwani kwa kufanya hivyo kutaathiri chaguzi zijazo hasa uchaguzi mkuu mwaka 2020. Hii imeelezwa kwa sababu, wakurugenzi wa wilaya hutumiwa kama wasimamizi wa chaguzi zilizopo chini ya wilaya husika.
Waliongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutakuwa hakuna uwanja sawa wa ushindani kwani upande mmoja utakuwa unapendelewa zaidi.
Wakiendelea kutoa maoni yao walitanabaisha kuwa ni dhahiri kuwa sasa hakuna utengano kati ya siasa na utendaji chini ya serikali ya awamu ya tano kwani Rais ameamua kujaza wanaomtii ili kujiwekea mazingira mazuri kwenye uchaguzi ujao.
Ufanisi serikali utapungua kwani nafasi za utendaji wamepewa wanasiasa ambao hawana ujuzi wa nyadhifa hizo bali wao wanaunga unga tu, walisema wanaharakati hao.
Wengine waliohiji watumishi wa umma na watumishi wa serikali kupewa nyadhifa za kisiasa mfano wanajeshi. Sheria inapinga hili lakini Rais Magufuli anafanya atakalo kwa sababu katiba imempa mamlaka makubwa.
Kiongozi mmoja wa chama cha upinzani ambaye hakutaka kutajwa jina alihoji suala la mtu kutangazwa ameteuliwa lakini baada ya dakika chache unasiki uteuzi umetengulia. Aidha, alieleza kuwa hili linaonyesha serikali haina umakini na inafanya mambo kwa kukurupuka.
Wanaharakati wameeleza kuwa JPM amehodhi madaraka yote, kazi za wizara anafanya yeye, kila kitu anafanya yeye kitu ambacho ni kinyume na sheria za nchi yetu.
Kwa pamoja walihitimisha kwa kusema kuwa kikubwa ni serikali kufuata sheria, kanuni na taratibu kama haitafanya hivyo hawatachoka kuikosoa hadi pale itakapokaa kwenye mstari ulionyooka.
Post a Comment
Powered by Blogger.