Haya Hapa Mambo 11 Yanayofanya Watu Wengi Wasiendelee Maishani Mwao.

Zifuatazo ni tabia za kuachana nazo endapo unahisi unayo au unazo:-
  1. Kukaa kimya mahali ambapo hutakiwi kukaa kimya
Unafumbia macho yote unayoyaona, husemi chochote. Inaweza ikawa ni vizuri katika kazi upande wa wafanyakazi wenzio kosa linapotokea, lakini ukumbuke inaweza kukurudisha nyuma kwa kuwa watu hawatakufikiria katika chochote na kusema kwamba huna unalolijua. Hii ni tabia isiyofaa, achana nayo mapema. Acha sauti yako isikike, watu watambue uwezo wako.
  1. Uchelewaji
Wote tunaweza kusema tunamfahamu mtu mmoja kati ya watu wanaotuzunguka mbae kila siku yeye ni mchelewaje, katika maswala yote. Kwa upande wa kazi, uchelewaji hautakiwi. Kufika sehemu umechelewa kunakufanya uonekane hujali na usietegemewa.
  1. Unashikwa na kinyongo
Haina tatizo kama kuna mtu humfurahii au jambo limetokea na halijakufurahisha, ni kawaida kwa mwanadamu, lakini kubakiwa na kinyongo ni kujimalizia muda wako wa maana na nguvu zako za kufanya vitu vingine vya maana. Jifunze kusamehe na kusahau haraka.
  1. Kujilinganisha na mtu mwingi kwa namna yoyote.
Ulipokua mdogo uliwaza sana ni rafiki yupi na yupi mnaendana sana achana na hizo hisia kwa sasa, we ni mtu mzima na mwenye malengo yako, achana kabisa na mawazo ya nani anafikiria nini au yuko sawa na mimi. Fanya kazi yako, utimize malengo yako.
  1. Matumizi yako ni makubwa kuliko kipato chako.
Kama pesa kila siku zikiingia mfukoni huoni zinapoishia, jiangalie sana utaishia kuwa mtu wa aina hiyo kw amuda mrefu. Kuhifadhi pesa ni muhim sana kwa ajili ya maisha yako ya badae.
  1. Kutokufanya maamuzi
Kutokufanya maamuzi, kutokufanya maamuzi sahihi au kuamua kufanya maamuzi wakati mwingine kunakupotezea muda, pesa na zaidi kabisa heshima kwa watu wanaokuzunguka. Hii ni rahisi sana, maana suluhu ni kuwa mkweli. Achana kabisa na tabia ya kusema uongo hata kama uongo ni mdogo kiasi gani, kwa maana mazoea hujenga tabia.
  1. Kuongea bila kufikiria kwa makini
Ni muhimu sana kuwa mhalisia, lakini haimaanishi uwe unaongea bila kufikiria kwa makini chochote kile kinachokuja kichwani mwako. Ni tabia mbaya ambayo inaweza kukufanya uonekane ni mwenye jeuri, na usiyejua kitu.
  1. Usikivu Mdogo Kutokuufuata Maagizo.
Kuzungumza umbea sio vizuri kazini, naamini siku ukigundulika wewe ndo mbea wa ofisi hutajisikia vizuri tena kuenda kazini kila siku, utachukia kazi na wakati mwingine kusema umbea kunaweza kuharibu mahusiano ya kikazi baina ya wafanyakazi na mabosi.
  1. Ulalamishi
Kwa kuwa tunashauriwa kusema chochote kinachotutatiza katika mazingira ya kazi, na ni bora zaidi ili tuweze kuweka mazingira ya kazi salama, ila angalia usijijengee picha ya ulalamishi, jitahidi kumezea vitu vidogo.
  1. Umbea.
Wingi wa mawazo unaweza kuwa sababu kubwa sana ya mtu kutokusikiliza anachoambiwa na hauwezi kumzuia mwanadamu kuwa na mawazo, lakini kuna watu wengine huamua kutokusikiliza kwa makini au kufanya kile alichoelekezwa kwa makusudi. Unapoingia kazini acha vyote ambavyo vinakutatiza nje ya geti, unamuda mwigni sana wa kuwaza baada ya kazi.

Credit: Salma Mrisho
Post a Comment
Powered by Blogger.