Hatimaye Mwandishi Aomba Radhi Kwa Kusema Mlima Kilimanjaro Upo Kenya.


Mwandishi wa Associated Press, Cara Anna Julai 18, 2016 aliandika habari kuhusu taarifa ya kifo cha mpanda mlima Kilimanjaro na kusema mlima huo upo nchini Kenya.
IMG_20160720_004032
Jambo hili lilizua mtafaruku katika mitandao ya kijamii na Watanzania wengi wakitaka mwandishi huyo kuomba msamaha na kurekebisha habari hiyo kwani mlima Kilimanjaro upo Tanzania na si Kenya.
2e111d17d2034977bf3c83f84c8bc757Gugu Zulu, mpanda mlima aliyefariki akipanda mlima Kilimanjaro.
Siku mbili baadae, Julai 20, jarida hilo limerekebisha taarifa hiyo kuwa kukiri kuwa mwandishi alikosea na kuwa mlima Kilimanjari upo Tanzania na si Kenya kama ilivyoelezwa katika habari ya awali.
IMG_-u96z83
Mpanda mlima huyo alifariki alipokuwa akipanda mlima Kilimanjaro katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela ili kuchangisha fedha za kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu nchini Afrika Kusini.
Hii si mara ya kwanza kwa vivutio vya asili vya Tanzania kusemekana kuwa vipo nhini Kenya kwani mara kadhaa tumewashuhudia hata wananchi wa Kenya wakisema vivutio vya Tanzania kama Olduvai Gorge vipo nchini Kenya.
Post a Comment
Powered by Blogger.