Hatimaye Jokate 'Kidoti' Afunguka Huku Akitoa Machozi.

Jokate Mwegelo 'Kidoti'
Mwanamitindo ‘the big name Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameibuka na kusema kuwa uvumilivu alionao na kujichanganya na watu unakaribia kumshinda kwa sababu unawapa nafasi kumtukana mitandaoni hivyo anawaonya kwani amechoshwa na hali hiyo.

Akizungumza na Wikienda, Jokate alifunguka kuwa anachukizwa na watu wanaotukana wenzao mitandaoni ndiyo maana uvumilivu ulimshinda na kujikuta akimtolea uvivu mtu aliyekibeza kidoti chake, akamjibu ndivyo sivyo.
“Unajua tunawapenda sana mashabiki wetu lakini kuna wakati wanatukosea, unakuta mtu ametoka alipotoka anakukomentia kitu ambacho siyo, kiukweli sitakubali kutukanwa, mimi ni mpole lakini sipendi upole wangu unifanye kutukanwa tu, nitachukua hatua,” alisema Jokate.
Hivi karibuni Jokate alitupia picha yake mtandaoni ya pozi la uso ambapo mtu mmoja akamuuliza kama ni kidoti au upele ndipo alipompa jina ambalo lilionekana ni tusi.

Chanzo:GPL
Post a Comment
Powered by Blogger.