Donald Trump Atoa Neno Kuhusu Uharifu Na Kumshtuma Mpinzani Wake.
Akiongea katika kongamano kuu la
chama cha Reublican wakati wa hotuba yake ya kukubali uteuzi, mgombea
huyo amesema hakuwezi kuwa na ufanisi bila kuwepo utawala wa sheria.
Aidha, ameahidi kuchukua hatua kali kukabiliana na wahamiaji haramu na akaonga kuwa kwa sasa wahamiaji wanaruhusiwa kuingia na kuishi katika jamii za Marekani bila kuzingatia usalama wa umma.
Bw Trump amejieleza kama mkombozi na sauti ya wanyonge na watu waliosahaulika nchini Marekani, na akajionyesha kama mtu mwenye sifa tofauti na mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton ambaye sana amemuonesha kama mtu mfisadi na asiyewajibika.
Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka Marekani amesema atakomesha sera ya kujenga mataifa na kufanikisha mageuzi ya serikali katika nchi nyingine ambayo amesema imefeli.
Amesema sera hiyo ndiyo chanzo cha matatizo yanayoshuhudiwa nchini Iraq, Libya, Misri na Syria
Ameahidi kufanya kazi na washirika wote wa Marekani wanaotaka kuangamiza kundi la Islamic State.