Diamond PLatnumz Aula Uingereza Awa Balozi Wa Vijana.

Diamond Platnumz.
SIKU moja baada ya kuachia wimbo wake mpya unaoitwa Kidogo aliolishirikisha kundi la P Square kutoka Nigeria, nyota wa kimataifa wa muziki nchini, Diamond Platnumz, ameteuliwa na Ubalozi wa Uingereza kuwa Balozi wa vijana.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose, alisema kupitia mradi wake unaoitwa Next Generation Tanzania, Diamond ataweza kuhamasisha vijana kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Ni mtu mwenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya Tanzania. Kupitia mradi huu ambao umedhamiria kuanzisha miradi na fursa nyingi kwa vijana wa kizazi cha leo na kesho hapa Tanzania watanufaika nao yeye atakuwa balozi,” alisema Dianna.
Post a Comment
Powered by Blogger.