Baada Ya Kupigwa Pini Na TFF,Jerry Murro Acharuka Na Kutoa Neno.

Msemaji wa Yanga Jerry Muro.
Taarifa zilizotoka jana  kwenye kamati ya nidhamu ya shirikisho la mpira wa mguu [TFF] kuwa limemfungia msemaji wa klabu ya Yanga Jerry Muro mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni tatu kutojishughulisha na masuala ya mpira kwa makosa mawili kushindwa kulipa faini na kulishambulia shirikisho hilo kwenye vyombo vya habari siku ya mechi ya TP Mazembe.
Kufuatia kufungiwa kwake hatimaye leo Murro ameibuka na kusema kuwa hatambui kufungiwa kwake kwa kuwa yeye ni mwajiriwa wa Yanga na si TFF kwa hiyo ataendelea kuwa msemaji wa Yanga milele na milele.
Akizungumza kutoka kwao Machame aliko kwenye mapumziko ya likizo anakiri kuwa barua walimpelekea klabu hapo,waliambiwa kuwa yupo likizo na wakaamua kumhukum bila ya yeye kuwepo na amesisitiza kuwa Tff hawana mamlaka ya kumfungia mtu pekee wa kumsimamisha ni Yanga ambao ni wajiri wake kuna mengi ataendelea kuyasema atakaporudi kazini.

Post a Comment
Powered by Blogger.