Al-Shabab Wavamia Kituo Cha Polisi.

Polisi nchini Kenya wanasema kuwa zaidi ya wapiganaji 100 wamevamia kituo kimoja cha polisi kaskazini mashariki mwa Kenya.
Wanasema wapiganaji wa al-Shabab waliingia mji wa Wajir wakiwa katika malori matatu saa za alfajiri siku ya Jumamosi.

Walirusha makombora ya roketi kabla ya kuondoka na silaha na magwanda ya polisi.
Polisi mmoja alijeruhiwa.Wapiganaji wa al-Shabab hutekeleza uvamizi wa mara kwa mara nchini Kenya ,mara nyengine wakivuka mpaka kutoka Somalia.
Kundi hilo pi lina wanachama wake wanaoishi nchini Kenya.
Post a Comment
Powered by Blogger.