Al-Shabab Waua Maafisa 4 Wa Polisi.

Maafisa wanne wa polisi wanahofiwa kufariki baada ya mtu mshukiwa wa ugaidi kumpokonya askari bunduki na kuwafyatulia maafisa wa Polisi.
Yamkini mshukiwa huyo wa ugaidi alikuwa amefungiwa korokoroni baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kujaribu kuwashawishi watu kujiunga na mtandao wa kigaidi wa Al Shabaab.
Alipelekwa katika kituo cha polisi cha Kapenguria, Kaskazini Magharibi mwa Kenya.
Awali gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa mtu huyo anadaiwa kuvamia kituo hicho kumnusuru mshukiwa aliyekuwa amekamatwa kwa tuhuma za ugaidi .
Gazeti hilo linasema huenda maafisa hadi watano wameuawa.
Mkuu wa polisi wa kituo hicho Vitalis Ochido anadaiwa kujeruhiwa.
Ufyatulianaji wa risasi bado unaendelea.
Tovuti ya habari ya Capital FM imemnukuu mkuu wa polisi Joseph Boinnet akisema polisi zaidi wametumwa eneo hilo.
“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anazuiliwa alitwaa bunduki na kuanza kuvyatua risasi," Bw Boinnet amenukuliwa. "Kituo hicho sasa kimezingirwa na juhudi za kukabiliana naye (mshambuliaji) zinaendelea."
Post a Comment
Powered by Blogger.