Kwa Mara Ya Kwanza Tangu Avunjike Mguu Vibaya,Demba Ba Asema Maneno Haya Kuhusu Soka..

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Demba Ba amesema hataacha kucheza soka hata baada ya kuvunjika mguu akicheza.Ba, ambaye kwa sasa huchezea Shanghai Shenhua, alivunjika mguu baada ya kukabwa akicheza mechi ya Ligi Kuu ya Uchina.
Baada ya mechi hiyo, mkufunzi wa mshambuliaji huyo wa Senegal Gregorio Manzano alisema jeraha hilo “huenda likafikisha kikomo uchezaji wake”.
"Hili ni jeraha mbaya sana lakini ninaweza kujikwamua. Sitafikisha kikomo uchezaji wangu hapa, hilo nina uhakika nalo,” amesema Ba, mwenye umri wa miaka 31.
“Msimu hapa unamalizika Novemba na kuanza Machi. Nitajizatiti kurejea kwa wakati kwa msimu utakaofuata.
Demba Ba alichezea West Ham, Newcastle na Chelsea katika Ligi ya Premia.
Alijiunga na Shenhua kutoka klabu ya Besiktas ya Uturuki, akinunuliwa takriban pauni 12 milioni mwezi Julai mwaka jana.
Kwa sasa, ndiye mfungaji mabao bora Ligi Kuu ya Uchina akiwa na magoli 14 kutoka mechi 18.

Post a Comment
Powered by Blogger.