AINA YA WATU WANAOHARIBU MAPENZI..Katika mahusiano kabla hujaingia ni lazima umshirikishe rafiki au ndugu yako wa karibu lakini potelea yote moyo wako lazima ulizie kuaza mahusiano na huyo mtu ambaye unatarajia kuwa naye tukumbuke kuwa mahusiano ni ya wawili na pia hayaangalii kabila,umri.umbile au,kipato japo wengi husema lazima uangalie vitu kama hivyo ili kujiridhisha na nafsi yako lakini pia kati ya watu utakapokuwa una tembea naye wakushangae kuwa una tembea|kuhusiana kimahusiano na mwanamke au mwanaume mnzuri.
Mungu ndiye mgawaridhiki,unzuri na makabila pia kwani kuna msemo unaosema mfungwa hachagui gereza laity kama mfungwa angekuwa anachagua wapi akafungwe basi wa Tanzania wangeomba kufungwa china au nchi yeyote nzuri nje ya nchi hii, ndivyo ilivyo kwenye mapenzi kuna makabila,maumbile au kipato cha mtu kinafanya kuwa ajute sana  kwanini alikuwa hivyo ni kwa sababu tu ya maneno ya watu juu ya kabila au vitu vingine ambavyo vinamfanya ashindwa kufurahia mahusiano.. 


Watu wanaochangia mahusiano ya watu kuharibika au kutodumu bila kugombana.

MARAFIKI
Hao ni watu ambao huwa wa kwanza kuharibu mahusiano ya watu wako radhi kufanya chochote ili tu kuona hamko sawa katika mahusiano na lengo laweza kutaka kuona wapenzi hao wanaachana ni swali gumu kwa wengi je,kweli rafiki yamgu kipenzi anaweza nifanyia hivi kunigombanisha na mpenzi wangu? Ukweli ni kwamba rafiki yako anaweza kukugombanisha vizuri tu na mwandani wako kama hauko makini tunabidi kutoamini sana marafiki katika mahusiano yamkini anaweza kuwa kigeugeu kati yenu ili kuwaharibu kabisa wawili nyiye matukio mengi ya kuachana marafiki huwa wakuchochea sana ili watu waachane na pia mpe mpenzi wako nafasi katika jambo Fulani ulilolisikia juu ya mpenzi wako.

NDUGU
Hakuna maisha ambayo mtu utakosa ndugu yaweza kuwa ndugu kutoka kwa upande wa bibi mdogo babu mdogo nk, hao wote ni ndugu zetu nakuamini kuwa ndugu sio ule uliyezaliwa naye tu hawa huwa ni vichochezi nakutoa kassoro nyingi kwa mtu ambaye analetwa kutambulishwa nyumbani kwanza huaza na miguno( mmh) ndo wifi|shemeji mmh jamani aya hongera lakini mmh yani hutafuta sababu tu wa kuanzisha majabizano na ukikosea kuwapa nafasi kuuliza kuna nini utaaza kusikia kasoro watakazo zitoa na wakimalizia ‘kweli mapenzi ni upofu mmh ‘ kitu ambacho wengi huaza kufikiria sana na kukosea kuwapa nafasi ndugu zao kuwafanyia maamuzi katika mahusiano na kuishia kumuumiza mtu kwa faida tu ya ndugu.

WAZAZI
Tunajua fika bila wazazi yamkini tusingelijua jua,mwenzi,au nyota na mbalamwenzi lakini wazazi wengi wameumiza mioyo ya watoto wao na hata wale waliowezwa kuachwa sababu ukiuliza atakuambia ‘isingelikuwa mama \baba Yake hakika angenioa’ lakini pia jibu utasikia kwa mtenda ‘kiukweli sikumpenda niliona si chaguo la mwanangu na licha ya hivyo kuna kasoro nimeona kwahiyo nisingependa awe mkwe wangu’ wazazi huacha majeraha kwa wengi na ata kusababisha wengi kujiua au kushuka thamani kwa kuharibika kisaikolojia.


Mzazi,Ndugu,Rafiki kamwe usiwe chanzo cha mtu Fulani kuharibu mahusiano yake kumbuka chozi lake la siku moja laweza kuwa laana katika maisha yako ata kwa miaka kumi amini kuwa mahusiano ni ya watu wawili walioridhiana kwa kila jambo bila kuangalia kasoro zao wenyewe yaani wamehamua kubebana kwa kila hali wanahitaji tu Baraka zenu na kuwarekebisha kidogo walipokosea lakini huna haki kumwambia hakika hutakiwi kuoa|kuolewa na mtu huyu mpe nafasi ya kuchagua kwani ni mtu mzima anajua lipi baya na lipi nzuri katika maisha yake yeye mwenyewe,…
Post a Comment
Powered by Blogger.