Zijue Timu Ambazo Zina Nafasi Ya Kutinga Robo Fainali,Bale Na Rooney Vitani Leo Euro 2016.


WAKATI michuano ya Euro 2016 inaingia katika michezo ya mwisho ya makundi ni vikosi gani na nini kinahitaji ili vitinge hatua ya 16?
Mpaka sasa ni vikosi vitatu pekee vilivyokwishatinga hatua ya 16 bora (mtoano), ambavyo ni Italia, Hispania na wenyeji Ufaransa, zikiwa zimebakia nafasi 13 kukamilisha timu zinazotakiwa kwenye hatua hiyo.
Kumbuka timu mbili za juu zitatinga hatua ya mtoano, wakati timu nne zitakazoshika nafasi ya tatu na kuzidi nyingine kwa pointi zitaingia katika hatua hiyo ya 16 bora.
Ikitokea timu mbili au zaidi zitalingana pointi katika nafasi moja kwenye makundi, taratibu kadhaa zitafuatwa.
Moja ya taratibu hizo ni kuangalia pointi, tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kundi A
Ufaransa- Wameshafuzu hatua ya 16, lakini walihitaji pointi moja dhidi ya Uswisi katika mechi yao ya jana.
Uswisi- Wana uhakika wa kuwemo tatu bora kwenye kundi lao, kwenye mchezo wao wa jana wakifanikiwa kushinda dhidi ya Ufaransa watakuwa vinara wa Kundi A. Ila watamaliza nafasi ya pili kama Romania watashindwa kuifunga Albania.
Romania- Lazima waifunge Albania kuweza kupata nafasi ya kutinga 16 bora, huenda wakashika nafasi ya pili kama Uswisi wakipoteza dhidi ya Ufaransa. Rekodi ya mabao itatumika kama Romania wakishinda 1-0 dhidi ya Albania na Uswisi wakifungwa na Ufaransa kwa bao moja, lakini kama wote wanalingana kwa mabao (kwa sasa wote wamefunga mabao mawili).
Albania – Wakifanikiwa kuifunga Romania, watakuwa na pointi tatu, wataweza kusonga mbele kama pointi hizo tatu zitaweza kuzizidi timu nyingine nne zilizoshika nafasi ya tatu. (Mechi zote za Kundi A zilitarajiwa kufanyika jana).

Kundi B
England – Wana uhakika wa kumaliza nafasi tatu za juu. Watakuwa vinara wa makundi wa Kundi B kama wataifunga Slovakia kwenye mchezo wao wa leo mjini St Etienne, hata wakipata pointi moja itawafanya kukaa kileleni kama Wales hawataifunga Urusi, kwenye mechi nyingi ya kundi hilo itakayofanyika leo.
England wanaweza kushika nafasi ya tatu kama wakifungwa na Slovakia na Wales wakaifunga Urusi.
Wales – Watakuwa nafasi ya pili kama wataifunga Urusi, pia wanaweza kuwepo kwenye nafasi hiyo kama Slovakia hawataifunga England.
Kama Wales wataifunga Urusi na England kushindwa kuichapa Slovakia, kikosi hicho cha Chris Coleman kitakuwa kinara wa kundi hilo. Ila watamaliza nafasi ya tatu kama watatoka sare dhidi ya Urusi.
Slovakia – Watafuzu kama watashinda dhidi ya England na watamaliza nafasi ya pili kama Urusi wataifunga Wales.
Pia kuna uwezekano wa Slovakia kutolewa kwa kushika nafasi ya nne kama watapoteza na Urusi wakashinda.
Urusi – Wanahitaji kushinda dhidi ya Wales ili wasonge mbele. Kama wakiifunga Wales na England kupoteza, Urusi na England zitashika nafasi ya pili na ya tatu itategemea na tofauti ya mabao.

Kundi C
Ujerumani- Wakipata sare dhidi ya Ireland Kaskazini watakuwa wamefuzu na hiyo pia itawatosha kuwa vinara wa Kundi C, kama Poland wakishindwa kuifunga Ukraine. Kama Poland wataifunga Ukraine na Ujerumani wakitoka sare, Ujerumani itamaliza nafasi ya pili dhidi ya Poland, pia wanaweza kumaliza nafasi ya tatu kama watafungwa na Poland kushinda.

Poland – Wanahitaji sare dhidi ya Ukraine kwenye mechi zao za kesho kupata nafasi ya pili, ikiwa watafungwa na Ireland Kaskazini wakapata sare dhidi ya Ujerumani itawafanya washike nafasi ya tatu. Poland watamaliza wakiwa vinara wa Kundi kama watashinda na Ujerumani kufungwa.
Ireland Kaskazini – Hawawezi kumaliza chini ya nafasi ya tatu, lakini watamaliza nafasi ya pili ya Kundi C kama wataifunga Ujerumani. Watakuwa vinara wa kundi kama watashinda dhidi ya Ujerumani na Poland kushindwa kuifunga Ukraine.
Wakipata pointi moja pekee itawafanya washike nafasi ya tatu, ambapo wakipata pointi nne zitawasaidia kufuzu hatua ya 16 bora kwa kuwa kati ya timu nne bora zilizoshika nafasi ya tatu. Hata wakifungwa watashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi tatu, ambapo itawafanya wafuzu.
Ukraine – Watakuwa timu ya kwanza kutolewa kwenye michuano ya Euro 2016. Hata kama wataifunga Poland na Ireland Kaskazini kufungwa, watamaliza nafasi ya mwisho kutokana na matokeo waliyoyapata dhidi ya Ireland Kaskazini.

Kundi D
Hispania – Wamefuzu hatua ya 16 bora na wanahitaji pointi moja dhidi ya Croatia katika mchezo wao wa kesho Jumanne  ili kuwa vinara wa Kundi D.
Croatia – Watafuzu Kundi D wakipata pointi moja dhidi ya Hispania, wanaweza kuipiku Hispania kama wataifunga. Croatia watamaliza nafasi ya tatu kama watafungwa na Jamhuri ya Czech wakiifunga Uturuki, ambapo watawazidi kwa tofauti ya mabao.
Jamhuri ya Czech – Lazima waifunge Uturuki na kusubiria Croatia wafungwe na Hispania kuweza kumaliza nafasi ya pili ya Kundi D. Wakifunga katika nafasi ya pili dhidi ya Croatia taratibu za kuangalia matokeo ya mechi zao yatatumika. Ikiwa watamaliza nafasi ya tatu watakuwa na kazi ngumu kuweza kuwemo kati ya timu nne bora zitakazotinga hatua ya mtoano.
Uturuki- Nafasi yao ya pekee kufuzu ni kuwafunga Jamhuri ya Czech na kuwa na matumaini kwamba pointi zao tatu zitawatosha kushika nafasi ya tatu.

Kundi E
Italia – Wametinga hatua ya 16 bora na kuwa vinara wa makundi kwa kuwafunga Ubelgiji, ambao ndio pekee wanaweza kuwafikia kwa pointi.
Ubelgiji- Watamaliza nafasi ya tatu kama watatoka sare dhidi ya Sweden katika mechi yao ya Jumatano. Watamaliza nafasi ya tatu wakiwa na pointi tatu kama watafungwa, pia wanaweza wakamaliza nafasi ya nne kama watafungwa na Ireland wakimfunga Italia.
Sweden – Watapata nafasi ya tatu kama wakishinda na kama Sweden na Ireland watashinda pia, vikosi viwili vitatenganishwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Sweden watakuwa wametolewa kama hawatashinda.
Ireland – Wanalazimika kushinda ili kuweza kutinga 16 bora. Watamaliza nafasi ya pili kama watashinda na Sweden wakishinda, lakini kama watakuwa juu kwa mabao dhidi ya Sweden.

Kundi F
Hungary – Watamaliza wakiwa vinara wa Kundi F wakishinda dhidi ya Ureno, ila hata wakitoka sare kama Iceland watashindwa kuifunga Austria. Watamaliza wakiwa nafasi ya pili kama watafungwa na Ureno na Iceland wakishindwa kuibuka na ushindi, pia wanaweza kumaliza nafasi ya tatu kama wakipoteza na Iceland akishinda. Wana uhakika na kupata angalau nafasi ya tatu na wakiwa na pointi zao nne wanaweza kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 16 kama moja ya timu nne bora zilizoshika nafasi ya tatu.
Iceland – Watafuzu kama vinara wa Kundi F wakiifunga Austria na Hungary akipoteza dhidi ya Ureno. Kama Iceland watashinda na Hungary kutoka sare, Iceland watafuzu wakiwa nafasi ya pili, ila pia wanaweza kuwa nafasi ya kwanza kama watawazidi Hungary kwa tofauti ya mabao. Kama Iceland atapoteza na Ureno kushinda, watamaliza wakiwa nafasi ya nne, lakini wanaweza wakatinga 16 bora wakiwa na pointi tatu kama wakitoka sare na Austria na Ureno wakiizidi Hungary.

Ureno- Wanahitaji kushinda dhidi ya Hungary katika mechi yao ya Jumatano ili waweze kusonga mbele na hata kuwa vinara wa kundi kama Iceland watashindwa kuifunga Austria. Kama wakishinda na Iceland akashinda, Ureno wanapaswa kuwa zaidi ya Iceland kwa mabao ili kuweza kumaliza wakiwa kileleni. Kulingana kwa pointi kwa Ureno na Iceland kwasasa wakiwa wanafanana kwa tofauti ya mabao, watagombea nafasi ya pili au ya tatu lakini wataangalia mabao waliyoshinda.
Austria – Wanaweza wakamaliza nafasi mbili za juu kwa kuifunga Iceland na Ureno wakiifunga Hungary. Kama Ureno watashinda, Austria hawawezi kushika nafasi ya pili, lakini wakishinda dhidi ya Iceland kutawapa pointi nne wakiwa nafasi ya tatu, watakuwa kwenye nafasi ya tatu na kuwa na makali ya kuweza kuwa kati ya timu nne zitakazofuzu kwa kushika nafasi ya tatu zikiwa na pointi nyingi zaidi ya nyingine.

Post a Comment
Powered by Blogger.