YANGA YANASA SAINI YA MSHAMBULIAJI HATARI,JE TAMBWE AU NGOMA KUWEKWA BENCHI?

Mchezaji mpya wa Yanga Obrey Chirwa akisaini.

Obrey Chirwa ambaye yupo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini umri wa miaka 23 cha Zambia, anakuwa staa wa tatu kujiunga na Yanga akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, baada ya Donald Ngoma na Thabani Kamusoko kusajili na wao wakitokea klabu hiyo msimu uliopita.
Chirwa akiwa na Donald Ngoma.
 Mchezaji huyo ameshawahi kupelekwa kwa mkopo katika ligi ya Sweden katika timu inayoshiriki ligi kuu ya humo na alifaulu majaribio ila timu hiyo ilitowa dau dogo ambalo halikuwalidhisha viongozi wa Platinum na akaamuliwa arudi katika timu yake mpaka sasa alikuwa anaongoza kwa ufungaji huku timu yake ikiwa inaongoza ligi baada ya kucheza mechi 6 yeye akiwa amefunga jumla ya mabao 4.
Chirwa ni mchezaji anayecheza mbele yaani katika nafasi ya ushambuliaji au winga na Yanga wanafanya juhudi za kupata kibali cha Caf ili aweze kucheza katika mechi yake na TP Mazembe mchezo utakaochezwa.
Huu ni mwendelezo wa kocha wa Yanga Pluijm kupendekezwa kusajiliwa kwa mchezaji huyu kutokana na kocha kumkubali kwa kiwango chake kupitia kwa mawakala na pia ataleta changamoto kwa Ngoma na Tambwe.
Post a Comment
Powered by Blogger.