YANGA KUFA AU KUPONA KESHO DHIDI YA WAARABU?


                                                              Timu inayotamba kwa kucheza vizuri katika michezo katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga kesho itakuwa ugenini kucheza na waarabu wa Algeria timu ya Mo Bejaia katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika majira ya saa nne na kwa ukanda wa Afrika mashariki itakuwa saa sita usiku.
Yanga ambao walikuwa wameweka kambi nchini Uturuki kwa wiki moja sasa tayari wametua nchini na Algeria huku wakiwa matumaini ya kupata ushindi na kuweka rekodi kwa timu za kiarabu ikumbukwe kuwa Yanga hawajawahi kupata ushindi dhidi ya Waaarabu.
Kwa upande wa kocha Mkuu wa timu hiyo Hans Van De Pluijm amesema tayari ameshajua mbinu za wapinzani wake na tayari amewapa maelekezo wachezaji wake na kinachosubiliwa na mechi yenyewe.
'' Amesema kuwa'tupo tayari kwa kuchukua ushindi huu kwani tumejiandaa vizuri kwa hatutawaangusha watanzania wanaosubiri ushindi  kwa hamu' pia  alisema wao kwa sasa wana uzoefu katika mashindano hayo na kuwa wanajua ugumu wa mechi''Pluijm.
Yanga.
    

Post a Comment
Powered by Blogger.