YANGA KILIO KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA NA TP MAZEMBE MWENDO KASI.

Yanga.

Mabingwa wa ligi kuu ya  Vodacom na wawakilishi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki klabu Ya Yanga imeanza vibaya katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kupokea kichapo cha bao moja bila majibu toka kwa wenyeji timu ya Mo Bejaia.
Mchezo ulianza kwa kasi huku wenyeji wakilisakama lango la wageni kama nyuki mnamo dakika ya 18 wenyeji walipata bao kwa shuti kali na baada ya kuingia kwa bao hilo Yanga waliliandama lango la Mo Bejaia mara kwa mara umakini kutoka kwa washambuliaji waliokuwa wanaongozwa na Ngoma na Tambwe walishindwa kutumia vizuri nafasi hizo.
Yanga walipata pigo baada ya beki wao kuumia Osca Joshua na nafasi yake ilichukuliwa na Haji Mwinyi hadi mapumziko Mo Bejaia walikuwa wanaongoza bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza na mnamo dakika ya 8 mpira ulisimama kutokana na mashabiki kuwasha maguruneti na kumulika tochi kwa mlinda mlango wa Yanga na dakika ya 89 Haji Mwinyi alioneshwa kadi nyekundu hadi dk 90 Mo Bejaia wameibuka na ushindi wa 1-0.
Na matokeo mengine katika kundi hilo TP Mazembe wakiwa nyumbani wameutumia vyema uwanja wao kwa kuwafunga Madeama toka Ghana kwa mabao 3-1.
Yanga watalazimika kuzikata kilomita 6120 kurejea kwao Tanzania kabla ya kujipanga kukutana na Kisiki kingine TP Mazembe ya DRC katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne au Jumatano kati ya 28/29..

Post a Comment
Powered by Blogger.