Masuala Matano Muhimu yaliyoibuka Wakati wa Mahojiano ya Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe na Polisi, Leo Jijini Dar es salaam.
  1. Maombi ya Chama Cha ACT Wazalendo ya mkutano ilikuwa ‘Kujenga Chama’ Lakini Chama Kilizindua “Operesheni Linda Demokrasia” (Operesheni ambayo Ni Sehemu ya Ujenzi wa Chama, Maana Kama Demokrasia ikiachwa iteketezwe Na Serikali ya Rais Magufuli, bila Kulindwa, Basi hata Uwepo wa Vyama Vingi Utakuwa Mashakani).
2. Kusema “Rais Ameropoka kuhusu Sakata la Sukari Nchini” (Kwa kuelezea Namna alivyoueleza Umma akiwa Babati Kuwa Kuna Sukari imefichwa Na kukamatwa Mbagala, Taarifa ambazo TRA na Takukuru walizikanusha na Kusema Sukari Husika haikuwa imefichwa).