Vitendo Vya Unyanyasaji Vyawaliza Wafanyabiashara Soko La Samaki Jijini Mwanza

 Wafanyabiashara wa Soko kuu la Samaki na  matunda Jijini Mwanza, wameangua vilio kufuatia  vitendo vya  unyanyasaji dhidi yao, vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa Soko hilo vikiwemo vipigo pamoja na kufichiwa matoroli ya kufanyia usafi.
Kutokana na mgogoro huo uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja, Wafanyabiashara hao wamelazimika kukutana na kuiomba Serikali kuingilia kati sakata hilo, ili kurejesha amani ya Soko iliyoanza kutoweka katika siku za hivi karibuni.
Katika sakata hilo Wafanyabiashara hao wameiambia seetheafrica.com kuwa, mgogoro huo umeibuka baada ya viongozi hao kuwalazimisha wafanyabiashara hao wakusanye fedha kutoka kwa Wafanyabiashara wenzao, ili waweze kuwapatia viongozi hao
Wakati mgogoro huo ukichomoza, kumbukumbu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela, alipata fursa ya kutembelea Soko hilo ambapo aliagiza kuwa Wafanyabiashara hao wasibugudhiwe wala kuhamishwa katika eneo hilo.
Post a Comment
Powered by Blogger.