Video | Mvutano Waendelea Baina Ya Chadema Na Polisi Wilayani Kahama

Polisi wilayani Kahama mkoa Shinyanga ililazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA pamoja na viongozi wao katika uwanja wa CDT  mjini Kahama baada ya kukaidi agizo la kutofanya mkutano.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kwamba wakati jeshi la polisi likifyatua mabomu hali ilikuwa tete katika uwanja wa CDT kwani wananchi walilazimika kutimua mbio bila kujali hali ya usalama wao ambapo eneo hilo liligubikwa na moshi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho mh Mbowe amelani vikali tukio hilo. 
 
Post a Comment
Powered by Blogger.