Usipitwe Na Hii Je Wajua Mwangaza Mwingi Huathiri Binadamu?

Utafiti wa wanasayansi unaotumia data kutoka kwa satelaiti na vipimo vya ardhini umebaini kuwa zaidi ya 80% ya watu ulimwenguni wanaishi chini ya anga iliochafuliwa na mwangaza.
Uchafuzi huo unasemekana kusababishwa na mwangaza bandia barabarani, nyumbani na pia mwangaza wa taa za magari.

Singapore, Kuwait na Qatar hushuhudia mwangaza mwingi zaidi nyakati za usiku, huku Jamhuri ya Afrika ya kati, Chad na Madagascar zikiwa na mwangaza mdogo zaidi.
Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la Science Advances journal, unaonya kuwa ukosefu wa giza la kutosha nyakati za usiku utaongeza visa vya matatizo ya kulala kwa binadamu.

Post a Comment
Powered by Blogger.