Ujue Ugonjwa Wa Sumu Kuvu Ulioibuka Dodoma Na Athari Zake

 Na Dorcas Safiel Sumu kuvu ni aina ya kemikali  za sumu inayozalisha ukungu au fangasi wanaota kwenye mbegu za nafakaa zinazoota kwenye mahindi, mbegu za kunde,mbegu za mafuta au hupatikana pia kwenye mazao ya mifugo kama chakula kimechafuliwa na sumu hiyo au maziwa ya mama anayenyonyesha aliyetumia chakula chenye sumu hiyo.. 
Sumu kuvu haionekani kwa macho, haina harufu, haina rangi,wala kionjo ni jambo ambalo linakuwa gumu kujua kama ugonjwa huo umevamia nafaka yako., ukungu unatokana na sumu kuvu unaweza kuwa rangi ya kijani,rangi ya chungwa,kijivu, njano chafu au kutoa harufu ya uvundo.
 Ukungu unaotoa sumu kuvu ustawi ikiwa mazao yamekubwa na ukame yakiwa bado shambani na kushambuliwa na wadudu wa haribifu na kuhifadhiwa kwenye ghala lenye joto au lenye unyevu wa kiwango cha juu kabisa, mfano mpunga ambao ukiweka kwenye sehemu yenye unyevu kwa muda mrefu hubadilika na kuwa kijivu.
 Vyakula vinavyoweza kuambukiza sumu kuvu ni mahindi na unga wake, karanga na mazao yanayotokana na karanga; muhogo; nyama; mayai,maziwa pamoja na vyakula vya mifugo vinavyotengenezwa.
 binadamu au mnyama huweza kula sumu kuvu kupitia vyakula vilivyoathiriwa na kemikali hiyo.

 Kwa tafiti za kisayansi hizi ni Athari za sumu kuvu.

  Nchi ya Tanzania ikiwa ni ya kitropiki lakini ugonjwa huu ulikuja kwa kasi kwa mwaka 2014 na kuibuka tena mwaka 2016 mkoani dodoma na kufanya watu kushangaa kwa kutokujua nini cha kufanya ikiwa bado ugonjwa huu unaweza kuepukika kwani kuna maeneo maalum ya kuhifadhi chakula ili kisiweze kukaa kwenye unyevu na kupata sumu kuvu na serikali inabidi itoe elimu hasa kwa maeneo ya vijijini kwani ndiko ugonjwa huu ulipoaza kuibuka na kuwafanya watu kuwa na mashaka kwa kuua haraka.
Post a Comment
Powered by Blogger.