Ubabe Kenya Yapeleka Jeshi Lake Nchini Somalia.

Kenya imetuma kikosi kikubwa cha jeshi hadi katika mpaka wake na Somalia.
Ripoti kutoka Nairobi zinasema kuwa, idadi kubwa ya maafisa wa jeshi, na magari yao ya kivita, wameonekana wakielekea katika eneo la Bula-Hawa katika Wilaya ya Gedo nchini Somalia.
Nia ya kikosi hicho kikubwa kutumwa Somalia bado haijabainika, lakini kuna tetesi kuwa huenda Kenya ikarejea na mipango yake ya awali ya kujenga ukuta wa usalama kaskazini mwa nchi hiyo, mpakani na Somalia.
Taarifa za kuaminika zinasema kuwa mpaka kati ya nchi hizo mbili kaskazini mwa Kenya umefungwa.
Serikali ya Kenya na Somalia bado hazijasema lolote.
Post a Comment
Powered by Blogger.