#ThrowBackThursday Mjue Jean Marc Bosman Mwanasoka Aliyevurugwa Na Maisha Ya Soka.

 Leo katika throwback Thursday tunakuletea au tunakukumbusha kuhusu mtu anaitwa jean Marc bosman unamfahamu huyu mtu au umeshawahi hata kumsikia?au unafahamu nn kuhusu Jean marc Bosman basi kama hufahamu lolote ondoa tone la shaka mimi nipo hapa kwaajiri yako.
Hivi umeshawahi kusikia suala la mchezaji kuhama kutoka timu moja kwenda timu nyingine akiwa huru? Natumai umeshwahi kusikia sana kwa timu yako kununua mchezaji ambaye hana mkataba au kumuachia mchezaji ambaye hana mkataba kwa kiingereza wakiita free transifer je Free transifer ni kitu gani haswa?
Free transifer ni kitendo cha timu kumuachia mchezaji ambaye mktaba wake umefikia mwishoni au timu kumuweka mchezaji kwaajiri ya manunuzi hasa mkataba wake unapokaribia kufika mwishoni na tendo hili au sheria hii kwa jina lingine ndo huitwa the bosman Transifer
Lakini najua unajiuliza kwann imeitwa Bossman transifer huyu Bosman ni nani haswaaa au ni kitu gani?
 JEAN MARC BOSMAN huyu ni mchezaji wa kimataifa wa ubeligiji ambaye ambaye kila ukifika mwezi October tarehe 30 ndo maulidi yake akizaliwa 1964 huko ubelgiji.
Ulikuwa ni msimu wa 1990 wakati huo Bosman akiichezea Royal football club iliyokuwa na makazi yake Liege maarufu kama  RFC Liege mktaba wake ulikuwa unaelekea kumalizika yani ulikuwa unaelekea mwishoni n a miaka yake miwili ndani ya timu hyo haikwenda vile ambavyo yeye ametarajia na akapata shavu kutoka ufaransa la timu ya daraja la pili ya Dunkirk lakini RFC Liege hawakuwa tayari kumuachia bosman kwani hawakupata kiasi cha fedha walichotarajia
RFC Liege  sio tu hawakumuongezea mktaba na kumnyima fursa ya kwenda nchini ufaransa alikopata dili bora zaidi lakini pia waliamua kumpunguzia mshahara.Maisha ya soka ya Bosman yalivurugwa kabisa kwani chama cha soka cha ubelgiji kilimfungia kwa kugoma kusaini mkataba na hakuna timu iliyokuwa inamtaka kwa wakati huo.
Jean Marc Bosman hakukubaliana na hali hyo na akisaidiana na wanasheria wake Luc Mission na Jean Luis Dupont wakipeleka suala hili katika mahakama ya usuruhishi the EUROPEAN COURT OF JUSTICE dhid ya chama cha soka cha aubeligiji timu ya RFC na Shirikisho la soka barani ulaya UEFA wakisimamia mktaba wa Roma wa mwaka 1957 au Treaty of Rome ambao ulikuwa unatanabaisha kuwa mchezaji yeyote ana uhuru wa kutoka timu moja kwenda timu nyingine  barani ulaya.
Na najua unajiuliza je kwani kabla ya hapo hali ilikuwaje? Kabla ya Bosman rule mchezaji alikuwa hawezi kuondoka ndani ya timu hata kama mkataba wake utamalizika labda mpaka timu yake ikubli kumuuza au wapate pesa nzuri ambyo wataridhika nayo kutoka timu ambayo inamtaka kwahyo kwa kiasi kikubwa ni suala ambalo lilikuwa linamktandamiza mchezaji.
Bosman na wanasheria walifanya kazi usiku na mchana lakini kwake kilikuwa ni kipindi kigumu sana katika maisha yake ya soka lakini walikuwa wanajua sio tu wanachokifnya lakini pia walichokuwa wanakitaka.na mwaka 1995 Jean marc Bosman alishinda kesi.
Je nini kilitokea baada ya ushindi wa Bosman?
Na sio tu alishinda kesi dhidi ya mamlaka kubwa katika soka lakini ulikuwa una maana ya ushindi wa jamiii ya wapenda soka kote duniani.
Kwanza Ushindi  ulikuwa unamaanisha mchezaji sasa  sio tu alikuwa yupo huru kuhama timu yake ikiwa mkataba wake utmalizika bila kusubiri ruhusa kutoka kwa timu yake lakini pia ana uhuru wa kutaka kiasi chochote cha pesa anacho kihitaji kutoka kwa timu yake au timu ile inayomuhitaji kwasababu kulikuwa hakuna ada ya uhamiisho.

Sir Alex Ferguson alishawahi kunukuliwa akisema  alichokifanya Bosman ni kitendo cha kishujaa na ameleta uhuru ameleta freedom ya kutosha kwaajiri ya watu wote duniani wenye mapenzi ya dhati na soka.
Waswahili wanasema aisifiyae mvua jua imemnyea kabla ya Bosman Rule kuja kulikuwa na sheria inatwa three plus two rule amabyo ilikuwa inasema timu hapaswi kuweka wacheaji watatu wa kigeni katika mechi na suala hili lilimgharimu Sir Alex Ferguson kwani wachezaji wa Scotland na Wales pia walihesabika wageni na kusababisha Sir ALEX asimpange golikipa Shmaiko golini badala yake alimuingiza  garry Walsh na Man united wakachezea kichapo cha manne kwa sufuli dhidi ya Barclona mwaka 1994.
Ebu fikiria maisha ya wachezaji hawa bila bosman rule yanguaje? Wachezaji kama Edger Davis na Patrick Kluivert kutoka Ajax kwenda Ac Milan,
Msimu wa 2001 Solcampbell alitoka tottenham hotspurs kwenda kwa mahasimu wa Arsenal ambapo aliweka mfukono paundi 60,000 na huku akiweka mfukoni bonus na marupurupu mengine kiasi cha paund mil 2 kwa mwaka.
Unakumbuka uhamisho waMichael Balack utoka Bayern Munich kwenda Chelsea 200? Robert  Levandoski kutoka Dortimkund kwenda Bayern munich 2014?,Andrea pirlo kutoka juventus Ac Milan kwenda Juventus 2011? Brendan Rodgers alimchukua James Milner kutoka man city kwa hisani ya mzee Bosman hao ni huko majuu lakini hapa nyumbani kulivyokuwa na mizengwe hivi umeyafikiria maisha ya Hassan Kessy wa Simba kama sio Bossman rule?
Najua utakuwa unajiuliza sasa yeye amefaidika namna gani?
Ukweli ni kuwa hakuna pesa ambayo inaweza kulipa kile ambacho mzee  Jean Marc Bosman alichoufanyia mpira wa miguu na japo amelipwa kifuta jasho cha paund mil 312000 mwaka 1998 bado mwenyewe anasema bado anasubiri pongezi kutoka kwa wachezaji matajiri kama David Bekham,Cristiano RONALDO NA Lionel Messi nakwasababu shkurani ni jambo jema sana linalofanya lile jambo bora ndani ya mioyo ya watu kuwa ni la kwetu  pia  bakwa niaba ya ya Vuruga ya 102.5 Choice Fm tunashukuru sana kwa ushujaa wako.
Post a Comment
Powered by Blogger.