Thomas Ulimwengu Atoa Neno Kwa Yanga Kuhusu Salum Telela.

Mchezaji wa TP Mazembe Thomas Ulimwengu.


Ulimwengu
Ile ‘ishu’ ya Salum Telela kutoongezwa mkataba mpya mpya (kutemwa) na klabu ya Yanga imeendelea ku-trend kwenye mitandao ya kijamii nah ii ni baada ya nyota wa Tanzania Thomas Ulimwengu anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kuandika ujumbe kwenye akaunti yake ya instagram akielezea hisia zake juu ya Telela kutoswa kwenye kikosi cha Yanga.
Ujumbe uliondikwa na Ulimwengu kupitia akaunti yake ya Insta unasomeka hivi: “Mi namwita kiraka@abo Master…sijawahi kumwona akicheza golikipa tu ila sehemu zote anakava… tuko pamoja mwanagu#hainakufeli #hainakufeli ….”
Kabla ya Ulimwengu, Juma Abdul pia ali-post kupitia akaunti yake ya Instagram na kutoa ya moyoni baada ya rafikiyake kutopewa mkataba mwingine wa kuitumikia Yanga mara baada ya ule wa awali kumalizika.

Telela hayupo kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Uturuki kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya mchezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia, lakini uongozi wa Yanga haujatoa taarifa rasmi ya kuachana na kiungo huyo aliyedumu kwenye klabu hiyo kwa misimu sita mfululizo.
Post a Comment
Powered by Blogger.