Tazama Matokeo Ya COPA AMERICA Kundi D,Argentina Yalipa Kisasi Na Bolivia Hoi.

Michuano ya Copa America imeendelea tena leo nchini Marekani hii ikiwa kundi D ambapo timu mbili zilicheza katika mfululizo wa hatua ya makundi na mechi ya kwanza imechezwa saa 03;00 usiku majira ya Africa Mashariki kati ya Panama na Bolivia na mchezo huu Panama wameibuka na ushindi wa 2-1.
Blas Perez.
Alikuwa mshambuliaji tegemeo katika timu ya Panama Blas Perez aliyeipa ushindi timu yake alipofunga mabao yote mawili mnamo dakika ya 11 na 89 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Panama walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Wachezaji wa Panama wakishangilia.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kunako dakika ya 54 Bolivia walisawazisha bao kupitia kwa mshambuliaji wao Juan Carlos Arce na wengi wakiamini kuwa mchezo huu utaisha kwa sare dakika ya 89 Blas Perez alizima ndoto za sare za Bolivia alipoifungia timu yake bao la ushindi na kuipa pointi tatu muhimu Panama hadi mchezo unamalizika Panama 2-1.
Juan Carlos Arce.
Mchezo wa pili umeanza saa 05;00 kwa majira yetu mabingwa watetezi wa kombe hilo Chile walicheza na Argentina hii ikiwa kama fainali ya mwaka jana pale Chile walipowafunga kwa mkwanju wa penati na mchezo huu Argentina wamelipa kisasi cha fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Angel Di Maria.
Alikuwa winga hatari Angel Di Maria mnamo dakika ya 51 kipindi cha pili aliiandikia bao timu yake hii kutokana na kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare na katika dakika ya 59 Argentina walipata bao la pili na la ushindi kupitia kwa Ever Banega.
Ever Banega.
Chile walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Fabian Orellana dakika ya 90 hadi kipenga cha mwamuzi kinamalizika Argentina wameweza kulipa kisasi na kuibuka na ushindi wa 2-1.
Fabian Orellan akiwa na Rojo beki wa Argentina.

Post a Comment
Powered by Blogger.