Tazama MANENO MUME ALIVYOMWAMBIA MKE WAKE USIKU BAADA YA HARUSI YAO.

MANENO MUME ALIYOMWAMBIA MKE WAKE USIKU BAADA YA SHEREHE YA HARUSI YAO.
‪#‎inasikitisha‬
"Mke wangu, watu wote wameenda nyumbani kwao , mziki umezimwa, shamrashamra zimeisha. Harusi yetu ilikua nzuri mno ila sasa imepita. Tumemaliza harusi sasa ni muda wa kujenga familia yetu. Tuliobaki baada ya harusi hii ni mimi na wewe tu peke yetu. Hatma ya kesho huanza leo. Maisha yetu sasa sio kama ya nyuma. Nakumbuka kuna kipindi ulivaa gauni jekundu, lilikupendeza sana, siku ile nlitaman kukugusa, tulikua kwenye maonyesho ya sinema nilikua na shauku kubwa sana kwako. Nilitamani japo kukusogeza upande wa chooni ili nikakubusu tu ila haikuwezekana. Niliumia sana moyoni. Ila sasa wajua nini siri ya furaha yangu? Jibu la siri ya furaha yangu ni kuwa sasa nimekupata, niko na wewe pamoja milele, naweza sasa kukubusu kila siku.
Kabla sijakuvua nguo na kufanya mapenzi na wewe kwanza ngoja nikuambie vitu vichache vya muhimu mno......... Sina cha kukuficha, kuanzia leo simu yangu waeza kuitumia kama yako pia waeza tumia account na profile zangu Facebook, whatsapp na instagram kama zako. Kuanzia leo nimekua mtoto. Miaka mitano iliyopita maishani mwangu nilikua mwanaume, niliamka asubuhi mapema mwenyewe, siku nyingine nililala na njaa, nilifanya kila kitu nilivyojisikia, nilirudi nyumbani mda niliotaka, ila yote hayo YAMEISHA LEO. 


Kuanzia leo umekua MAMA yangu ambaye utanikemea nitakapochelewa kurudi nyumbani, utakayeniamsha asubuhi mapema niwahi kazini na kuhakikisha silali na njaa hata siku moja.
Nina furaha kuu kuwa sasa ninaye MAMA ndani yako. Natumaini utakua mama mwema. Usiwe mkali nami nakuahidi sitokua msumbufu. Mda mwingine nitakuudhi ila nakuahidi nitakua mfariji wako na kuirejesha furaha yako. Wakati wazazi wangu walipofariki, niliwalea wadogo zangu, nilikua kama BABA kwao. Hivyo sitokua mbaya kuwa BABA kwako. Kuanzia leo nitakulea nikikujali na kukupigania kama BABA yako nawe ukinitunza kama MAMA yangu. Nakupenda sana, tuvumiliane na kudumisha upendo wetu daima hadi pale Mungu atakapotutenganisha"

Post a Comment
Powered by Blogger.