TAZAMA MAJIVUNO YA CRISTIAN RONALDO.
Cristian Ronald

Linaweza kuwa jambo la kukushangaza au pengine  hata kukutia hofu 
wakati mwingine itakulazimu tu uamini kuwa ‘ Sifa jipe mwenyewe, usingoje kupewa” na hii ndio aliyoitumia  mshambuliaji hatari wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo. 


Kwa wengine wanamchukulia Ronaldo kama mtu wa majivuno huku wengine wakitafsiri kujisifia kwake ni sifa ya mtu anayejiamini na ni moja ya mbinu binafsi ya kujishawishi kuongeza bidii ili kuendelea kuwa matawi ya juu. 

Ronaldo hajasita kujitangaza kwa mara nyingine tena kuwa yeye ni mchezaji bora na mara hii, amekwenda mbali zaidi na kujitangaza mchezaji bora zaidi duniani kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. 

Katika mahajiano na jarida la Undici la nchini Italia, Ronaldo amesema anaamini kuwa yeye ni mwanasoka bora zaidi katika kipindi cha miongo miwili iliyopita. ” Mimi ni mchezaji bora zaidi katika kipindi cha miaka 20, haya sio maoni yangu tu, hata matokeo na takwimu yanaonesha hivyo” ” Nimejituma sana kufikia kiwango cha juu ni,ichofikia, na bado naendelea kufanya hivyo. Naweka mkazo kwenye mazoezi sawa sawa na ninavyofanya kwenye mechi” Ameongezea kuwa kuwa bidii na juhudi vimemfikisha kileleni na ataendelea kuandika historia kwa miaka mingi ijayo.” Walio bora huandika historia katika michezo yao, nimefanya hivyo na nitaendelea kwa miaka mingi ijayo” 
Post a Comment
Powered by Blogger.