Tazama Maamuzi Ya Tume Ya Maridhiano Jinsi Yatakavyobuniwa Nchini Sudan Kusini.


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar wamependekeza kwamba taifa hilo linafaa kubuni tume ya ukweli na maridhiano kama ile ya Afrika Kusini ili kusaidia kuliponya taifa hilo baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wale watakaosema uhalifu wao watasamehewa.
Katika taarifa ya pamoja ilioandikwa katika gazeti la New York Times,wawili hao ambao hadi hivi majuzi walikuwa katika pande pinzani katika vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe,''walisema tuko tayari kuunganisha jamii zetu na kujenga umoja''.
Wamesema kuwa mpango wa kuwashtaki mahakamani wale wote waliotekeleza uhalifu utaathiri juhudi za kuunganisha taifa hilo kwa kuweka wazi hasira na chuki miongoni mwa raia wa Sudan Kusini.
Shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch limekosoa mapendekezo hayo kama juhudi za kukwepa haki.
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wawili hao walikubaliana kubuni mahakama itakayoungwa mkono na Umoja wa Afrika kuwashtaki wahalifu wa kivita.
Rais na makamu wa rais wameitaka jumuiya ya kimataifa kuangazia upya mpango huo.
Post a Comment
Powered by Blogger.