Tazama Hii Wanasayansi Wageuza Hewa Ya Sumu Kuwa Jiwe.

Watafiti wanaoendesha uchunguzi katika eneo la Iceland, wanaamini kuwa wanaweza kupunguza hewa chafu inayochafua mazingira kwa kunasa hewa ya sumu ya carbon dioxide na kuigeuza kuwa mawe.
Wanasayansi hao waliyeyusha hewa hiyo ndani ya maji kupuliza mchanganyiko wake ardhini, ambako ilichanganyika na madini ya volcano na kuunda mawe inayofanana na chokaa.
Wanasayansi hao wamesema mfumo huo unaweza kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya viwango vya joto duniani kwa sababu mawe ya volcano inayohitajika kugeuza gesi hiyo yanapatikana kote duniani.
Utafiti huo wa miaka miwili uligharimu takriban dola milioni 10m.
Wanapendekeza kuwa hiyo itakuwa njia dhabiti ya kupambana na tabia nchi japo itagharimu pesa nyingi.
Mradi huo unaotambuliwa kama CarbFix unaweza kunasa hewa ya sumu kutoka angani na kuipenyeza kupitia kwenye mabomba na maji hadi ardhini.
Shughuli hiyo inakamilika kwa asilimia 95% ya hewa hiyo kuganda na kuwa jiwe.
Post a Comment
Powered by Blogger.