TAZAMA HAPA TETEZI ZA SOKA ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMAMOSI YA LEO.

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 25.06.2016.

Mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez, 24, ameambiwa anaweza kuondoka Santiago Bernabeu na kwenda Old Trafford lakini ikiwa tu Manchester United watatoa pauni milioni 50 (Daily Mirror),

 Nafasi ya Rodriguez huenda ikazibwa na kiungo mchezeshaji wa West Ham Dimitri Payet, 29, ambaye Zinedine Zidane amesema mchezaji huyo anaweza kuwa mchezaji mzuri katika klabu yoyote Ulaya (Daily Mirror),
 Meneja mpya wa Manchester City Pep Guardiola amempigia simu kumpa moyo mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 21, ambaye amekuwa akisuasua kwenye michuano ya Euro. Sterling alizomewa na baadhi ya mashabiki wa England kwenye mchezo dhidi ya Wales, na hakuchezeshwa kwenye mechi dhidi ya Slovakia (Guardian), 
Nolito, 29, anayesakwa na Manchester City amekiambia kituo cha redio cha Marca kuwa „kwa sasa sijasaini Man City, lakini sidanganyi, tusubiri tuone.” City wako tayari kulipa pauni milioni 13.8 kumsajili mchezaji huyo wa Celta Vigo (Manchester Evening News),
 Mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku, 23, amesema anamuachia wakala wake kushughulikia mustakabali wake. Mchezaji huyo amehusishwa na kurejea Chelsea (Sky Sports), 

Meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte amepewa jukumu la kuirejesha Chelsea kwenye ‘Top Four’ baada ya klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya 10 msimu uliopita (Daily Mail), 

Sunderland, Manchester United, Everton na Southampton wanamfuatilia mchezaji wa kimataifa wa Uturuki Ozan Tufan, 21. Mchezaji huyo wa Fernabahce alifunga goli wakati Uturuki iliposhinda 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech kwenye michuano ya Euro (The Chronicle), 
Watford nao pia wameanza kumfuatilia winga wa Newcastle, Andros Twonsend, 24 (Daily Mirror),
 Mshambuliaji wa Manchester United Ashley Fletcher, 20, amekataa mkataba mpya wa kubakia Old Trafford. Aliichezea Burnley kwa mkopo msimu uliopita na huenda akahamia Leeds United (Yorkshire Evening Post),
 Mshambuliaji wa Everton Oumar Niasse, 26, ananyatiwa na Galatasaray (Talksport), 
Chelsea, Manchester United na Arsenal wote wanamtaka mshambuliaji wa kimataifa wa Spain Alvaro Morata, 23. Real Madrid wametumia haki yao ya kumnunua tena kutoka Juventus mapema wiki hii lakini wanaweza kumuuza tena (Squawka).
 Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Post a Comment
Powered by Blogger.