Tazama Hapa Matokeo Ya EURO Na COPA AMERICA,Lionel Messi Apiga 3.

Michuano ya Euro 2016 ilifunguliwa jana nchini Ufaransa kwa wenyeji timu ya Ufaransa ilicheza na timu ya Taifa ya Romania katika uwanja wa Stade De France na wenyeji waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Uwanja wa Stade De France.
Mchezo ulianza kwa Romania kukosa bao dakika ya 1 huku wenyeji wakicheza kwa kulishambulia lango la Romania ambao walicheza kwa kujilinda muda wote hadi mapumziko timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Olivier Giroud.
Alikuwa mshambuliaji wa timu ya Aresnal alipoanza kuifungia timu yake bao mnamo dakika ya 57 kwa krosi safi ya winga hatari wa West Ham Dimitri Payet na Romania hawakukata tamaa kunako dakika ya 65 walipata penati baada ya mlinzi wa zamani wa Man United Patricia Evra kucheza rafu na mwamuzi kuamua ipingwe penati na ilifungwa na Bogdan Stancu na kuisawazishia timu yake bao safi.
Bogdan Stancu akipiga penati.
Wafaransa walisubili kupata bao katika dakika ya lala salama kiungo aliye bora kwa sasa N'golo Kante alitoa pasi kwa Dimitri Payet aliyeweza kuachia shuti kali mnamo dakika ya 89 hadi mpira unamalizika wenyeji wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika kundi A.
Dimitri Payet na Olivier Giroud.
Michezo mengine itaendelea tena leo kundi A na B kucheza Albania watacheza na Uswis saa kumi jioni,na Saa moja usiku Wales watacheza na Slovakia na majira ya saa nne watacheza England watacheza na Urussi.

Katika bara la America kombe la Copa America Argentina wamefuzu Robo Fainali kwa kuibamiza Panama mabao 5-0 shukurani zote ziende kwa mshambuliaji bora wa Dunia Lionel Messi ameonesha ubora wake kwa kufunga hat trick.
Lionel Messi.
Mabao mengine yamefungwa na Nicolas Otamedi na Sergio Aguero hadi dakika 90 Argentina wameibuka na ushindi wa mabao 5-0.
Nicolas Otamedi.
Sergio Aguero.
Mchezo mwingine mabingwa watetezi wameibua matumaini ya kuingia robo fainali baada ya kuwatadika Bolivia Mabao 2-1 shukurani ziende kwa Arturo Vidal aliyefunga mabao yote.
Arturo Vidal.

Post a Comment
Powered by Blogger.