Tazama Hapa Matokeo Ya Copa America,Uruguay Yatupwa Nje,Mexico Haikamatiki.

Michuano ya Copa America imelindima tena leo usiku na Alfajiri kwa mechi mbili zilichezwa katika nchi ya Marekani ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza.
Mchezo wa kwanza ulikuwa Uruguay na Venezuela na matokeo ya mchezo huu Venezuela wameshinda bao 1-0 na kuwafanya kutinga robo fainali kwa kufikisha jumla ya pointi 6 sawa na Mexico na Uruguay imetupwa nje ya mashindano hayo huku ikisubili tu mchezo mmoja kwa heshima.
Mexico wameendeleza kugawa dozi baada kuwafunga Jamaica mabao 2-0 na kutinga hatua ya robo fainali ikiungana na Colombia na Venezuela walioendeleza na wimbi la ushindi.

Post a Comment
Powered by Blogger.