Tazama Hapa EURO Na COPA AMERICA.

Michuano ya Euro imeendelea tena kwa mechi tatu kupigwa nchini Ufaransa mchezo wa mapema uliwakutanisha mabingwa watetezi Hispania dhidi ya jamhuri ya Czech na mchezo huu Hispania wameanza vema baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 bao la dakika za lala salama likifungwa na beki Gerrard Pique kwa kichwa.

Mchezo wa pili uliwakutanisha Ireland na Sweden ambapo timu hizi zimetoka sare ya kufungana 1-1 huku mshambuliaji hatari Zlatan Ibrahimovic akishindwa kuipa ushindi timu yake.

Na mchezo wa uliofuata ulikuwa mkali na wakusisimua Italia na Ubelgiji na huu mchezo watu wengi waliamini Ubelgiji ataibuka mshindi cha ajabu alikutana na kichapo cha aibu baada ya kufungwa mabao 2-0 na Italia.
Nchini Marekani Copa America mechi mbili za kukamilisha ratiba ya kundi C ambapo tayari timu zilizofuzu kwenda robo fainali zinajulikana ni Mexico na Venezuela ambazo zilitoka sare ya 1-1 na kufungana kwa pointi 7 zikiwa tofauti ya kufungwa na kufunga na vibonde wa michuano hiyo timu ya Uruguay imeuona mwezi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamaica.
Post a Comment
Powered by Blogger.