TAASISI ZA KIBENKI TANZANIA KUKUTANA PAMOJA NA KUTOA ELIMU YA KIBENKI KWA WADAUDar es salaam, Maonyesho ya Taasisi za Kibenki 2016 (Tanzania Bankers Exhibition 2016) ambayo yameandaliwa na Imori International yanafanyika kwa siku nne (4) kuanzia tarehe 27 mpaka 29 Julai 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Maonyesho haya yanashirikisha Wakuu wa taasisi hizo, na wanategemea kuzungumzia fursa mbalimbali za kibiashara zilizopo, mipango ya uwekezaji na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.


Katika Maonyesho hayo atashiriki Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaju katika kufahamu fursa za kibiashara, uwekezaji, changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili sekta hiyo na kukaa pamoja na kujua ni kwa jinsi gani wanaweza kuzitazama na kuzitatua changamoto hizo, kushirikisha wadau mbalimbali ili kuhakikisha uchumi unakuwa katika hali nzuri ambayo itaweza kuinua maisha ya wananchi wanaoishi Tanzania katika kuhakikisha wanafaidika kupitia taasisi hizi.

Kwa asilimia ndogo ya Watanzania ndiyo wamekuwa wakitumia huduma za kibenki nah ii inatokana kwa sababu ya kukosa elimu ya kutosha, lakini kupitia Maonyesho haya ya Taasisi za Kibenki 2016 (Tanzania Bankers Expo 2016) wananchi watapata nafasi ya kupata elimu na kukutana kwa karibu na watumishi wa mabenki na kujenga ukaribu ili kuhakikisha wananchi wanatumia kikamilifu huduma za kibenki katika kusaidia ukuaji wa sekta ya fedha nchini.

Akongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa  Imori International  ambao ni waandaaji  wa Tanzania Bankers Exhibition, Ndugu Leo Nyanduga ameeleza kuwa maonyesho hayo ya kisekta yaliyodhamiria kuwa chachu kuu ya kukutanisha benki zote, taasisi zote za kifedha, taasisi zote zinazoweza kutoa huduma mbalimbali kwenye sekta hiyo, yatakuwa ni mwanzo wa kukuza zaidi sekta hiyo kikamilifu.

Amesema “maonyesho haya  (Tanzania Bankers Exhibition 2016) yatakuwa ni maonyesho yaletayo chachu katika sekta, kuwapa nafasi watu kujua namna taasisi hizi za kifedha zinavyoweza kutatua changamoto zao wakizitumia vyema”

“Hii ni nafasi ya kipekee katika sekta kwa kuwa kwa mara ya kwanza wasomi wa sekta hii watapata nafasi kuongea na wananchi na wale waliofanikiwa sana katika kuendesha taasis hizo za kifedha nchini, ilisisitizwa kuwa mashirika na kampuni ambazo mpaka sasa hazijakamilisha taratibu za ushiriki wafike katika ofisi zetu kukamilisha au watembelee tovuti ambayo ni  www.bankersexpo.co.tz ” Ameongeza.

 Wazungumzaji wengine ambao watazungumza katika tukio hilo ni pamoja na Naibu wa fedha na mipango Mhe. Ashatu Kijaji, Mwenyekiti wa Chama cha benki Tanzania, Dkt. Charles Kimei.

Post a Comment
Powered by Blogger.