SOMA HAPA TETESI ZA SOKA ZA USAJILI BARANI ULAYA IJUMAA YA LEO.Meneja mpya wa Manchester United Jose Mourinho anataka kuonesha makali yake ya usajili kwa kiungo wa Juventus Paul Pogba, 23, ndio kipaumbele cha juu (Manchester Evening News), 

Borussia Dortmund wamebadili mawazo na sasa wanasema Henrikh Mkhitaryan, 27, anayesakwa na Manchester United anaweza kuuzwa kwa pauni milioni 30.6. Mchezaji huyo kutoka Armenia amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake (Kicker), 

Liverpool wamekataa dau la pauni milioni 8 kutoka Swansea la kumtaka kiungo Joe Allen, aliyeondoka Swansea miaka minne iliyopita (Daily Mirror),

 Liverpool wataongeza juhudi zao za kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka Senegal, Sadio Mane, 24, kwa pauni milioni 30 wiki ijayo (Telegraph),

 Meneja wa zamani wa Nice, Claude Puel ameibuka kuwa kocha anayedhaniwa kuwa atachukua kazi ya umeneja Southampton (Telegraph),

 Manchester City wanamwania kiungo wa Dinamo Zagreb Ante Coric, 19, kwa pauni milioni 6. Mchezaji huyo yuko Ufaransa kwa sasa na kikosi cha timu ya taifa ya Croatia (Daily Mail),

 Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anamtaka beki wa Everton John Stones, 22, na ndio mchezaji anayempa kipaumbele zaidi katika usajili wake (Marca),

 Kiungo Samir Nasri, 28, atakuwa na mazungumzo na Pep Guardiola wiki ijayo, akitaka kuendelea kubakia Etihad (Daily Mirror),

Paris St-Germain wamemfukuza kazi meneja Laurent Blanc, na kumpa pauni milioni 16.85 za mkono wa kwaheri (L’Equipe), 

Watford wamempa mkataba mpya mshambuliaji wake Troy Deeney, 27, baada ya dau kutoka Leicester la pauni milioni 25 kukataliwa (Watford Observer), 

Leicester bado wanamtaka beki wa Burnley Michael Kane, 23, licha ya dau lao la awali la pauni milioni 10 kukataliwa (Leicester Mercury),

 Sunderland wanazungumza na Rubin Kazan ya Urusi ya kumsajili moja kwa moja kiungo Yann M’Vila, 25, aliyecheza kwa mkopo Sunderland msimu uliopita (Sunderland Echo), 

Stoke wamepanda dau la pauni milioni 19.6 kumtaka mshambuliaji Manolo Gabbiadini, 24 aliyepachika mabao tisa katika mechi 31 msimu uliopita (Daily Mirror). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa
Post a Comment
Powered by Blogger.