Silvio Berlusconi Apelekwa Hospitalini Kwa Tatizo La Moyo.

Aliyekuwa waziri mkuu nchni Italy Silvio Berlusconi amepelekwa hospitalini akiwa na tatizo la moyo ,kulingana na msemaji wa chama chake.
Berlusconi mwenye umri wa miaka 79 hatahivyo yuko katika hali nzuri,aliongezea.
Taarifa kutoka hospitali ya San Raffaele mjni Milan imesema kuwa kulazwa kwake kulikuwa muhimu baada ya tatizo hilo.
Bw Berlusconi alikuwa waziri mkuu wa Italy mara nne ,lakini ameshtakiwa kwa kukwepa kulipa kodi na kutoa hongo.
Kiongozi huyo wa Forza Italia ambaye alikuwa na miaka 70 alipowekwa mashini ya kusaidia moyo atafanyiwa ukaguzi katika siki chache zijazo,ilisema taarifa ya hospitali.
Post a Comment
Powered by Blogger.