SIKIA HII STAND UNITED KUISHTAKI TFF KWA FIFA.


Jengo-la-TFF1
TFF inatuhbumiwa na klabu ya Stand United ya mkoani Shinyanga kwamba haiungi mkono uongozi ambao ndiyo uliounda timu, badala yake na badala yake ina-support watu wacheche ambao wameingia kwenye timu hiyo baada ya udhamini kutoka ACACIA na kutaka kuwapoka timu wapiga debe wa Stand ili waiendeshe wao.
Mshauri wa masuala ya ufundi wa Stand United Dkt. Jonas Tiboroha amesema, ushahidi wote upo kati ya maafisa wa TFF na baadhi ya viongozi wa kundi ambalo haliungwi mkono na Stand United. Kama klabu, wameamua kupeleka ushahidi huo mbele (FIFA) ili kuona haki yao inapatikana.

“Sisi tumechukua documents zote ambazo zinahusisha mgogoro huu jinsi abavyo ulikuwa na jinsi ambavyo tunautafsiri kisheria, facts zaidi ya 26 na vielelezo zaidi ya 42 ambavyo tunavipeleka FIFA na tumepeleka kesi saba zinazoonesha namna gani Stand United inavyo nyang’anywa haki zake mkononina kundi la watu fulani,” anasema Dkt. Tiboroha Katibu Mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga.

“Wakati sisi tunafanya juhudi kufanya uchaguzi, kumbe kuna mawasiliano upande kwa pili nao wameambiwa pia wafanye uchaguzi, sasa mwisho wa siku TFF watatambua katika uchaguzi upi?”

Stand United imekuwa kwenye mvutano kwa muda mrefu mara baada ya kupata udhamini kutoka kwa kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA. Baada ya timu hiyo ya Shinyanga kupata udhamini mnono, zilianza kutengenezwa kamati mbalimbali kwa ajili ya kusimamia fedha hizo huku baadhi ya viongozi wa zamani wa timu hiyo wakiwekwa pembeni ya timu hali ambayo imezua mvutano mkubwa.
Post a Comment
Powered by Blogger.