Siasa Zetu Mahakama Kuu Kupinga Kuondolewa Rais Maduro.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.

Serikali ya Venezuela imeitaka mahakama kuu kupinga mapendekezo kutoka upande wa upinzani ya kutaka kupigwa kwa kura ya maoni ya kumtoa madarakani Rais Nicolas Maduro.

Afisa wa ngazi ya juu kutoka serikalini Jorge Rodriguez amewatuhumu viongozi wanaohusika katika kuratibu kura ya maoni kuwa ni wadanganyifu. Wiki iliyopita ,tume ya uchaguzi ya Venezuela ilitangaza kuwa ni zaidi ya sahihi laki sita zilisainiwa kiubadhilifu katika kupitisha kura ya maoni kwa sababu ya madai ambayo yalikiuka utaratibu. Upande wa upinzani wamesema kuwa mamlaka ya tume ina uependeleo baina yao.
 Kwa sasa Venezuela inayumba na kiuchumi kutokana na mfumuko mkubwa wa bei pamoja na ukosefu wa chakula na mahitaji muhimu.
Post a Comment
Powered by Blogger.