Serikali Ya Ufaransa Imesema Itatoa Dola Millioni 200 Kwa Uganda.

Serikali ya Ufaransa imesema itatoa dola milioni 200 kujenga barabara kati ya mji mkuu wa Uganda Kampala na mji wa kibiashara uliopo mashariki wa Jinja kulingana na gazeti la daily Monitor.
Ufadhili huo ambao unashirikisha asilimia 90 ya jumla ya fedha zote zinazohitajika kumaliza mradi huo zitatoka katika shirika la maedeleo ya ughaibuni la Ufaransa AFD.
Maafisa wa Uganda wanasema kuwa barabara hiyo itakuwa laini nne hadi nane katika maeneo mengine.
Kwa sasa hakuna barabara kama hiyo.

Barabara kati ya Jinja hadi Kampala ni mojwapo ya barabara ilio na biashara nyingi,ikiwa ndio inayotumika kwa biashara za kuuza bidhaa nje pamoja na tiafa la Rwanda ,Burundi na mashariki mwa DRC.
Ujenzi unatarajiwa kuanza mapema mwaka 2017 ijapokuwa umecheleweshwa tayari.
Post a Comment
Powered by Blogger.