RASMI VICTOR WANYAMA ASAINI TOTTENHAM.

Victor Wanyama.
Kiungo na Nahodha wa Harambee stars Victor Wanyama imekamilisha rasmi uhamisho wake wa kwenda Tottenham akitokea Southampton kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 11.
Kulikuwa na taarifa hizi hapo awali Sasa ni dhahiri Wanyama ni mchezaji wa Tottenhamn baada ya kusaini rasmi mkataba mrefu wa miaka mitano kuichezea klabu hiyo.
Wanyama alijiunga na Southampton mwaka 2013 akitokea Celtic ya Scotland kwa ada ya uhamisho ya kitita cha paundi milioni 12.5 akitokea Germinal Beerschot ya Ubelgiji.
Hadi sasa Victor Wanyama amefunga magoli manne katika mechi 85 alizochezea ligi kuu ya England.
Post a Comment
Powered by Blogger.