Rais Obama Leo Hii Kukutana Na Sanders Huku Akimsifia Hillary Clinton Na Kusema Neno Hili.
![]() |
Rais Obama. |
Matamshi yake yamejiri baada ya Hillary Clinton kushinda uteuzi wa chama hicho kuwania kiti cha urais, baada ya kushinda idadi ya wajumbe katika uteuzi wa Urais.
Obama ametaja Bi Clinton kama 'Kiranja shupavu' na wakati huo huo kumpongeza mpinzani wake Bernie Sanders kwa kuendesha kampeini na kujadili masuala muhimu ya kijamii.
Sanders ambaye hajakubali kushindwa, anatarajiwa kukutana na rais Obama baadaye hii leo.
Wakati huo huo Obama amesema jukumu lake kuu wakati wa kampeini za uchaguzi mkuu ni kuwakumbusha wapiga kura nchini Marekani, kuwa rais wa Marekani ni kazi ngumu na sio maonyesho ya runinga, hili likimlenga mgombea wa chama cha Republican Donald Trump.