Pierre-Emerick Aubameyang Ampiku Robert Lewandowski Na Kuwa Muafrika Wa Kwanza Kwa Tuzo Hii.

Mchezaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang.
Mchezaji kandanda bora barani Afrika wa mwaka huu Pierre-Emerick Aubameyang ametawazwa kuwa mshindi wa tuzo la mwaka huu la mchezaji bora katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga
Aubameyang ambaye ni raia wa Gabon na mshambulizi wa Borussia Dortmund alimpiku mshambulizi wa Bayern Munich Robert Lewandowski kwa asilimia 0.2%.
Tuzo hilo hutolewa na shirikisho la wachezaji nchini humo VDV.
''Ni furaha kubwa kutambuliwa na wachezaji wenzangu '' alisema Aubameyang
''Tuzo hii naipokea kwa niaba ya mashabiki wangu wote na mashabiki wa Dortmund ''

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Gabon amefunga mabao 25 na kusaidia 6 katika mechi 31 alizoshiriki msimu huu.
Msimu uliopita aliisaidia klabu yake kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Bayern Munich.
Aidha alifunga jumla ya mabao 39 katika mashindano yote na kumpa hadhi ya kuwa mchezaji mwafrika wa pekee aliyetajwa katika timu Bundesliga mbali na kuwa mwafrika wa kwanza kuwahi kutwaa taji hilo la VDV tangu liasisiwe.

Timu ya BundesligaWachezaji wengine waliotajwa katika kikosi cha msimu huu cha Bundesliga ni kipa Manuel Neuer (Bayern Munich)
walinzi: Mats Hummels (Bayern Munich), Jerome Boateng (Bayern Munich), David Alaba (Bayern Munich), Philipp Lahm (Bayern Munich)
Safu ya kati: Thomas Müller (Bayern Munich), Henrikh Mkhitaryan (Dortmund), Douglas Costa (Bayern Munich), Arturo Vidal (Bayern Munich)
Washambulizi : Robert Lewandowski (Bayern Munich), Pierre-Emerick Aubameyang (Dortmund)
Post a Comment
Powered by Blogger.