PICHA YA AWALI KWA TATHMINI NA MWELEKEO MICHUANO YA AFRIKA.

·
PICHA YA AWALI KWA TATHMINI NA MWELEKEO MICHUANO YA AFRIKA.
Hatimaye michuano ya vilabu hatua ya makundi barani Afrika imeanza mwishoni mwa juma lililoisha na yapo mambo ya msingi ya kujifunza na kuyafanyia kazi kwa wahusika wote.
Kwa jumla tathmini fupi ni kwamba kuna jumla ya vilabu 16 vinavyoshiriki hatua hii ya makundi ambapo ligi ya mabingwa ina jumla ya timu 8 ktk makundi mawili yaani A na B, vivyo hivyo ktk kombe la shirikisho kuna vilabu 8 pia ktk makundi mawili A na B yenye timu 4 kila moja.
Jumla ya michezo minane imepigwa ktk mashindano yote. 


LIGI YA MABINGWA
Jumla ya magoli 9 yalifungwa katika michezo minne ya ligi ya mabingwa iliyochezwa ktk makundi A na B.
Kundi A yalifungwa magoli 6 na kundi B magoli 3
Matokeo:-


Kundí A
Zesco 3-2 Al Ahly
Asec Mimosas 0-1 Wydad Casablanc.


Kundi B
ES Setif 0- 2 Mamelod Sundowns
Enyimba 0-1 El Zamalek
Katika ligi ya mabingwa ni timu moja tu iliyoshinda nyumbani nayo ni Zesco ya Zambia, lkn timu tatu zimeshinda ugenini nazo ni Wydad, Mamelod na Zamalek.
Mchezo uliozaa magoli mengi ni Zesco na Ahly kwa magoli 5 kufungwa na hii inaonyesha mchezo huu ulikuwa wazi.

KOMBE LA SHIRIKISHO
Kundi A
Tp Mazembe 3-1 Medeama
Mo Bejaia 1-0 Young Africans
Kundi B
KACM 2-1 Etoile du Sahel
FUS Rabat 1-0 Al Ahly Tripol
Katika michuano ya shirikisho nako magoli 9 yamefungwa huku kundi A likizalisha magoli 5 na kundi B magoli 4.
Lkn tofauti na ligi ya mabingwa kombe la shirikisho ktk makundi yote hakuna timu iliyoshinda ugenini na michezo mitatu kati ya minne tofauti ni goli moja isipokuwa mchezo mmoja kati ya Mazembe na Medeama.
Matukio muhimu.

1. Kati ya timu 16 zinazoshiriki michuano yote ni timu 5 tu zilizoshindwa kupachika walau bao moja ktk mchezo wa kwanza huku timu 11 zikifunga walau goli moja
2. Jumla ya magoli 18 yalitinga wavuni
3. Uwezo wa timu shiriki hauonekani kutofautiana sana
4. Maamuzi bado ni changamoto kwa ujumla wake
5. Michezo ya awali imeacha wazi hatima ya makundi yote na kuonyesha usawa wa nafasi ya kufanya vizuri
6. Hadi sasa inaonyesha hakuna timu ndogo ktk mashindano.

NB: Wapenzi wa soka na wachambuzi wajue kutofautisha kati ya matokeo na uhalisia wa mechi kwani hii ni ligi na siyo mtoano na ndo kwanza safari inaanza.

0717469593
Imani K Mbaga
Post a Comment
Powered by Blogger.